https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    WACHEZA SOKA 10 WANAOONGOZA KWA PESA DUNIANI

    Ronaldo & Messi
    Wote kwa pamoja Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kumi bora ya wachezaji wanolipwa vizuri zaidi ulimwenguni.
    Jarida la Forbes lilitoa orodha ya mwaka ya wacheza soka wanaolipwa vizuri zaidi, katika orodha ya wanamichezo 100, wanandinga waliochupa katika orodha hiyo ni 15. Wachezaji kama Steven Gerrard, Robin van Persie, Franck Ribery na Fernando Torres wametupwa nje ya orodha hiyo wakati wachezaji watano wa EPL hawapo katika listi kati ya wachezaji 10 bora wanaolipwa vizuri zaidi ulimwenguni.
    Orodha hii imehusisha majumuisho ya mishahara ya mwaka mzima na marupurupu wanayopata wachezaji hao.
    NB:#-Inawakilisha nafasi anayoshika kwenye orodha ya wanamichezo wote ulimwenguni.
    10) Luis Suarez (#73)
    Luis Suarez alikuwa na wakati mzuri katika msimu wake wa kwanza kabisa akiwa na klabu ya Barcelona na kufunga goli katika mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya na kuchukua ndoo ya michuano hiyo.
    Majumuisho ya pesa anayopata–Dola milioni 21 (Mshahara: Dola milioni 16.5, Marupurupu: Dola milioni 4.5)
    Luis Suarez kwa sasa ana thamni ya pauni milioni 43.5 endapo kuna klabu itahitaji huduma yake.
    9) Sergio Aguero (#45)
    Aguero alishinda kiatu cha dhahabu msimu uliopita Ligi kuu nchini Uingereza akifunga magoli 26.
    Jumla ya pesa anayopata: dola milioni 24.9 (mshahara– dola milioni 17.9, Marupurupu–dola milioni 7)
    Aguero ameshuka kwa nafasi moja kutoka  44 mpaka 45. 
    Puma wanampa Aguero pauni milioni 1.25 kwa mwaka. Makampuni mengine yanampa shavu ni pamoja na Pepsi, Gillette, Hugo Boss, Sony PlayStation na Samsung.
    8) Radamel Falcao (#38)
    Kiasi anachoingiza: dola milioni 25.9 (Mshahara–dola milioni 21.9, Marupurupu-dola milioni 4)
    Falcao ameshuka kutoka nafasi ya 15 mpaka ya 38 aliyokuwepo mwaka 2014. Sababu kubwa ni kutokana na kushuka kwa mshahara wake kutoka milioni 32.4 mpaka milioni 21.9
    Makampuni yanamdhamini ni pamoja na  Hublot  Gatorade, Samsung, Gillette na Panini.
    7) Wayne Rooney (#34)
    Rooney kwa sasa anapata pauni 300,000 kwa wiki 
    Mapato yake: dola milioni 26.9 (Mshahara–dola milioni 19.9, Marupurupu– dola milionin 7) 
    Amepanda kutoka nafasi ya #43  kwenda #34 mwaka huu
    Wadhamini wale ni pamoja na  HarperCollins, Nike Samsung, EA Sports na Coca Cola. Thamani yake kwa sasa ni Yuro milioni 45m.
    6) James Rodriguez (#27)
    Mapato yake: dola milionin 29 (Mshahara–dola milioni 24.5 kwa mwaka, Marupurupu – dola milioni 4.5)
    Wadhamini; 
    nguo za ndni za J10 ambazo zipo chini ya Bronzini Black, Adidas, Gatorade, Hugo Boss, Huawei na Pepsi.
    5) Neymar (#23)

    Only Ronaldo and Messi earn more than Neymar through endorsements.
    Mapato: dola milioni 31 [Mshahara – dola milioni 14m, Matangzao – dola milioni 17]
    Ameshuka kutoka nafasi ya #16 mwaka jana mpaka nafasi ya #23 mwaka huu.
    Wadhamini 
     Red Bull, Panasonic, Unilever, Volkswagen, Konami, Beats by Dre na, Nike. 
    4) Gareth Bale (#18)

    Mapato: dola milioni 35 (Mshahara – dola milioni 25.5, Marupurupu – dola milioni 9.5) 
    Ameshuka kutoka nafasi ya #14 mwaka jana mpaka nafasi ya #18 mwaka huu.
    Matangazo 
    Adidas, BT Sport na Lucozade.
    3) Zlatan Ibrahimovic (#14)

    Mapato: dola milioni 39.1  (Mshahara–dola milioni 33.1a mwaka, Marupurupu–dola milioni 6) 
    Ameshuka kutoka nafasi ya #12 mpaka ya #14 mwaka huu. 
    Matangazo 
    Adidas F50 Adizero Boots Dressman, Volvo na Xbox. Ana thamani ya Yuro milioni 15.
    2) Lionel Messi (#4)
    Mapato: dola milioni 73.8 (Mshahara-dola milioni 51.8, Marupurupu-$22m)
    Matangazo
    Adidas, Audemars Piguet, PepsiCo, Gillette,Turkish Airlines Vifaa vya umeme, Samsung 
    Thamani yake ni Yuro milioni 120.
    1) Cristiano Ronaldo (#3)

    Mapato: dola milioni 79.6 (Mshahara–dola milioni 52.6, Marupurupu–dola 27)
    Matangazo
    Nike, Tag Heuer na Emirates Airlines. Ana mashabiki milioni 102 na milioni 35 kwenye Twitter. Ana chupi zake mwenyewe na mashati yake yenye logo ya CR7.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WACHEZA SOKA 10 WANAOONGOZA KWA PESA DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top