Utafiti mpya umeonya kuwa robo ya
wanaume wote walio chini ya umri wa miaka 20 nchini China, watakufa
kabla ya kufikia umri mkubwa iwapo hawatoachana na tabia ya uvutaji
wa sigara.
Utafiti uliochapishwa katika jarida
la madaktari la The Lancet, umesema robo mbili ya wanaume nchini
China huanza kuvuta sigara wakiwa na umri wa miaka 20.
Kwa mujibu wa wanasayansi waliofanya
utafiti huo nusu ya wanaume hao watakufa kutokana na tabia ya kuvuta
sigara.
0 comments:
Post a Comment