https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    TANZANIA YAFUTA GUNDU LA MWAKA, YAIBAMIZA MALAWI 2-0 KUFUZU KOMBE A DUNIA


    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    TANZANIA imeshinda ya mechi ya kwanza mwaka huu, baada ya kuilaza Malawi mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa makundi ya kugombea tiketi ya Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018.
    Kwa ushindi huo, Taifa Stars iliyocheza mechi 11 bila ya ushindi mwaka huu, nane chini ya kocha aliyeondolewa, Mholanzi, Mart Nooij, imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga hatua ya mwisho ya mchujo, ambako itamenyana na Algeria.  
    Stars ambayo inafundishwa na mzalendo Charles Boniface Mkwasa, sasa itahitaji kwenda kulazimisha sare katika mchezo wa marudiano Jumapili mjini Blantyire.
    Mbwana Samatta (kulia) akipongezana na Thomas Ulimwengu baada ya bao la pili
    Thomas Ulimwengu akimiliki mpira mbele ya beki wa Malawi, Limbikani Mzava 

    Kiungo wa Tanzania, Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Malawi, Mivale Gabeya
    Mbwana Samatta akifunga baada ya kumlamba chenga kipa wa Malawi, Simplex Nthala 

    Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na Hagi Yebarow Wiish aliyesaidiwa na Hamza hagi Abdi na Salah Omar Abubakar wote wa Somalia, Taifa Stars ilikwenda kupumzika ikiwa tayari ina mabao hayo mawili kibindoni.
    Mabao yote yamefungwa na washambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Emmanuel Ulimwengu na Mbwana Ally Samata.
    Samatta alianza kufunga dakika ya 18 baada ya kumlamba chenga kipa wa Malawi, Simplex Nthala, kufuatia keosi- pasi ya Ulimwengu kutoka upande wa kulia.
    Ulimwengu akafunga la pili dakika ya 22 akiuwahi mpira uliotemwa na kip Nthala kufuatia krosi ya beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali.
    Stars ingeweza kurudi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ikiwa inaongoza kwa mabao zaidi, iwapo wachezaji wake wangetumia vizuri nafasi zaidi walizotengeneza.
    Kipa Ally Musafa Mtinge ‘Barthez’ aliokoa michomo miwili ya hatari ya Malawi kipindi cha kwanza, mmoja wa John Banda na mwingine wa Robin Ngalande.   
    Kipindi cha pili, Malawi inayofundishwa na mzalendo pia, Ernest Mtawali ilibadilika na kukataa kuruhusu mabao zaidi.
    Kwa mara nyingine, kipa Ally Barthez aliokoa michomo miwii ya hatari kipindi cha pili, wakati makali ya safu ya ushambuliaji wa Stars kipindi cha hicho yalipungua.
    Ushindi huo unaokuja siku moja baada ya Mkwasa kusiani Mkataba wa mwaka na nusu Taifa Stars- ni wa kwanza tangu aanze kazi Julai baada ya mechi nne, akitoa sare mbili 1-1 na Uganda, 0-0 na Nigeria na kufungwa 2-1 na Libya.
    Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Himid Mao, Thomas Ulimwengu/Ibrahim Hajib dk86, Said Ndemla, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa/Salum Telela dk69 na Farid Mussa/Simon Msuva dk80.
    Malawi; Simplex Nthala, Stanley Sanudi, Mivale Gabeya, Yamkani Fadya, Limbikani Mzava, Gerald Phiri, Chimango Kayira, Micium Mhone/Mamase Chiyasa dk46, Chawangiwa Kawanda, John Banda/Gabadinho Mhango dk58 na Robin Ngalande.  
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TANZANIA YAFUTA GUNDU LA MWAKA, YAIBAMIZA MALAWI 2-0 KUFUZU KOMBE A DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top