Hapa
ni katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga ambako jana
Jumanne,Oktoba 20,2015,wadau mbalimbali wa amani mkoani Shinyanga
wamekutana kwa ajili ya majadiliano ya ushirikiano wa kudumisha amani
katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2015.Kikao hicho kimeandaliwa na
uongozi wa mkoa wa Shinyanga likiwemo jeshi la polisi kwa kushirikiana
na Shirika la Save The Children linalojihusisha na utetezi wa haki za
watoto.
Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa ikiwemo kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto kabla,wakati na baada ya uchaguzi,lakini pia viongozi wa vyama vya siasa,wagombea na wanachama kuheshimu na kutekeleza sheria,kanuni,maadili na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi pamoja na sheria nyinginezo za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.
Mgeni
rasmi katika kikao hicho alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro
Rufunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa.
Fuatilia matukio katika picha hapa chini-Picha zote na Kadama
Malunde-Malunde1 blogMgeni
rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga
akifungua kikao hicho cha wadau ambapo pamoja na mambo mengine
alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kuona amani ya nchi inavurugwa
hivyo itachukua hatua kali za kisheria kwa watu wote watakaofanya vurugu
siku ya uchaguzi.Mgeni
rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga
akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ofisi yake imepata taarifa
kuwa kuna baadhi ya wagombea wanatembea na silaha za
moto,mapanga,manati na kufundisha vijana mbinu za kuvunja amani siku ya
uchaguzi.Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisisitiza kuwa watu wote
waliojiandikisha wana haki ya kupiga kura Oktoba 25,2015 na kuwataka
baadhi ya watu wanaojipanga kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura
kuachana na wazo hilo na badala yake waendelee tu shughuli zao na
wakati muda wa kutangazwa matokeo ndiyo warudi vituoniWadau
wa mkutano huo walisisitiza umuhimu wa wananchi kupiga kura kisha
kuendelea na shughuli zao Oktoba 25,2015 badala ya kukaa mita 200/300
kutoka kwenye kituo cha kupigia kura kwa vile kila chama kitakuwa na
wakala wake hao ndiyo wataweza kulinda kura zao .Kushoto ni kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga Justus KamugishaWadau
wakiwa ukumbini,kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro.Wadau wa amani mkoani Shinyanga pia walikubaliana kukabiliana na
watu wote wanaopanga kuvuruga amani ya nchi wakati wa uchaguzi.
Mwakilishi wa shirika la Save the Children Herman Mbunda akizungumzia umuhimu wa kulinda watoto wakati huu wa uchaguziKushoto ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng'umbi akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa(kulia)
Wadau
hao walikumbushana na kuhamasishana kulinda haki za watoto,wanawake na
makundi maalum katika jamii wakiwemo walemavu wakati wa uchaguziKikao kinaendeleaKikao kinaendeleaKikao
hicho cha wadau wa amani walisema ni vyema katika kipindi hiki cha
uchaguzi kila jambo linalofanyika basi kuwe na maslahi kwa watoto ambao
asilimia kubwa wanaingizwa katika masuala ya siasaWadau wa amani wakiwa ukumbiniKatibu
wa dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Pili
Misungwi(kushoto) akifuatilia kwa umakini zaidi kilichokuwa kinajiri
ukumbiniMkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede(kulia)Mkutano unaendeleaKikao cha wadau kinaendelea Mkutano unaendeleaWadau wakiwa ukumbiniViongozi wa dini wakiwa ukumbiniKikao kinaendeleaWadau wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbiniKaimu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mlimandago(kulia)Kikao kinaendeleaKikao kinaendeleaKikao kinaendeleaKamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akiwasilisha mada ya
ulinzi na usalama katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2015 ambapo
alisisitiza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na watu
watakaovuruga amani ya nchiKikao kinaendeleaKamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza katika kikao
hicho ambapo aliwataka waandishi wa habari nchini kutumia vizuri kalamu
zao ili kudumisha amani ya nchiWadau wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmiPicha ya pamoja washiriki wa kikao hichoWadau wakiwa katika picha ya pamoja Picha ya kumbukumbu Picha ya kumbukumbu Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment