Siku hii huadhimishwa kila tarehe 10 ya mwezi Oktoba ya kila mwaka na
maadhimisho ya mwaka huu 2015 yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Utu katika Afya ya Akili (Dignity in Mental Health)"
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tayari imetoa taarifa kuhusu maadhimisho hayo na moja ya mambo ambayo yameainishwa katika taarifa hiyo ya wizara ni pamoja na dalili zinazoashiria magonjwa ya akili ambazo nami nimeona ni vyema wewe msomaji wa www.dkmandai.com ukazifahamu kupitia hapa kama ifuatavyo:
Miongoni mwa dalili za kihisia ni pamoja na kukosa furaha na kuhuzunika sana, kuwa na furaha sana kupita kiasi, wasiwasi au woga kupita kiasi, kupunguza kuongea au kutokuongea kabisa au kuongea sana kupita kiasi, hasira za haraka haraka hata kufikia kupiga wengine na kuwa na msongo wa mawazo.

Dalili nyingine ni kujitenga na watu na kupenda kukaa mwenyewe muda
mwingi au kupenda kuwa na watu sana kuliko kawaida, kutokuwa na ari ya
kufanya kazi au kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila ya
kuzikamilisha, Kutokuonyesha hisia yoyote usoni mwake (mf. furaha au
huzuni nk), Kutokujijali usafi na muonekano waka pamoja na kuhisi maisha
hayana thamani na kuona bora kufa kuliko kuishi na hatimaye kufikia
uamuzi wa kujiua na hata kuua wengine.
Hizo zilikuwa ni dalili za kihisia kuhusu dalili za kimwi;i ni pamoja
na mwili kukosa nguvu au kuhisi mwili una nguvu sana kupita kiasi,
kukosa usingizi au kulala usingizi sana kupita kiasi, kukosa hamu ya
kula au kuwa na hamu sana ya kula, kutokutulia (kuhamanika) au kutulia
sehemu moja muda mrefu bila ya kujisogeza pamoja na maumivu sehemu
mbalimbali za mwili kama vile kichwa, mabega, mgongo, na viungo
mbalimbali ambavyo akienda hospitali vipimo havionyeshi tatizo lolote la
kimwili.
Dalili nyingine ni za kiakili ambazo ni pamoja na kukosa umakini wa
shughuli zako za kila siku, kusahau kwa haraka au kupoteza kumbukumbu,
kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa mitazamo tofauti, kusikia sauti
ambazo hazipo na kuona vitu ambavyo havipo, imani ya ajabu ambazo
haziendani na mila, imani au desturi za jamii yake ; kama vile yeye ni
mtu maarufu, au anaamini kuwa yeye ni nabii au anaamini kupokea taarifa
kutoka kwenye redio au mitandao ya simu
0 comments:
Post a Comment