RAIS Jakaya Kikwete, akitoa hotuba kwenye hafla ya kuweka jiwe la
msingi la kitegauchumi PPF Plaza eneo la Vigaeni, mjini Mtwara, Oktoba
10, 2015. Jengo hilo la ghorofa mali ya PPF litagharimu shilingi
Bilioni 9.5 ujenzi wake utakapokamilika mwishoni mwa mwaka huu.
NA K-VIS MEDIA, MTWARA
RAIS
Jakaya Kikwete ameumwagia sifa kemkem Mfuko wa Pensehni wa PPF, kwa
uwekezaji bora, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jingo la
ghrorofatano la kitegauchumi la PPF Plaza mjini Mtwara Oktoba 10, 2015.
“Nimefurahishwa
sana na uwekezaji wenu kwani ninaenda kustaafu na kupumzika kwa raha
kutokana na mambo makubwa mliyotafanya, nah ii ni fursa nzuri kwa
uwekezaji kwenye mkoa huu ambao utakuwa kitovu cha uchumi.” Alifafanua
Rais.
Rais
Kikwete, ambaye alitua mkoani humo akitokea nchi I Msumbiji alikokwenda
kuaga, alisema, Mtwara yuko muwekezaji ambaye ni tajiri mkubwa barani
Afrika akishikilia namba moja, nay eye angependa walau kulala mkoani
Mtwara wakati wa ziara zake za kukagua miradi yake, na lakini atalala
wapi, wakati hakuna hoteli yenye hadhi yake.? Aliuliza na kuwataka
wawekezaji zaidi katika eneo la mahoteli ili kuweza kuwapokea
wafanyabiashara wakubwa wanaotembelea Mtwara hivi sasa.
Akitoa
taarifa ya ujenzi huo, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF,
Aggrey Mlimuka, alisema, jingo hilo litakapokamilika ujenzi wake
litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 9.5 na tayari baadhi ya ghorofa
zimeshachukuliwa.
Rais
Jakaya Kikwete, (katikati), akipunga mkono kuwaaga wafanyakazi wa PPF na
wajenzi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko huo “PPF PLAZA” baada ya
kuweka jiwe la msingi
Rais
Jakaya Kikwete, akimkabidhi Subira Athumani, mfano wa kadi ya uanachama
kupitia mpango wa “Wote Scheme” ambao unahusu kujiunga na uanachama kwa
uchangiaji wa hiari. (Kushoto), ni Naibu waziri wa fedha, Adam Malima,
na wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo,
Aggrey Mlimuka
Naibu
Waziri wa Fedha, Adam Malima, akitoa hotuba kumkaribisha Rais Kikwete
kuweka jiwe la msingi la jingo la kitegauchumi la PPF mjini Mtwara
Oktoba 10, 2015
Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Aggrey
Mlimuka, akitoa hotuba wakati wa uwekaji jiwe la msingi la jingo la
kitegauchumi la Mfuko huo mjini Mtwara Oktoba 10, 2015
Baadhi ya
Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiongozwa na Makamu
Mwenyekiti wake, Aggrey Mlimuka, wakiwa katika picha ya pamoja na
Mwanachama mpya wa mpango wa uchagiaji wa hiari (Wote Scheme), wa Mfuko
huo, Subira Athumani Makumbiri, baada ya kukabidhiwa mfano wa kadi ya
uanachama
Ngoma za utamaduni nazo zilikuwepo kunogesha shughuli
Baadhi ya wafanyakazi wa PPF, na wajenzi, waimpungia mkono Rais na ujumbe wake wakati waiondoka eneo la tukio
Wajumbe
wa bodi ya wadhamini ya PPF, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi
hiyo, Aggrey Mlimuka, (wane kulia), na wafanyakazi wa PPF, wakiongozwa
na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, ambaye pia ni Mkurugenzi wa uwekezaji, Steven
Alfred (wakwanza kushoto mstari wa mbele)
Rais Jakaya Kikwete, (kushoto), akiangalia ushuhuda uliokuwa ukitolewa
na Mwanachama wa PPF kupitia mpango wa Wote Scheme, baada ya kuweka jiwe
la msingi la kitegauchumi la Mfuko huo mjini Mtwara Oktoba 10, 2015.
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, Aggrey
Mlimuka, Wakwanza kulia ni Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngoi, na
Meneja Uhusiano Lulu Mengele
Rais
Kikwete, na Mama Salma Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na naibu
waziri wa fedha, Adam Malima, Waziri wa Nishati, George Simbachawene,
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya
PPF, Wafanyakazi wa PPF, na wajenzi wa jingo la kitegauchumi la PPF
Plaza mjini Mtwara leo Oktoba 10, 2015. (Picha zote na K-VIS
MEDIA/Khalfan Sad)
Rais
Jakaya Kikwete, (katikati), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha, Adam
Malima, (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa
Pensheni wa PPF, Aggrey Mlimuka, wakati wa hafla ya uwekaji
jiwe la msingi kwenye jingo la kitegauchumi la Mfuko huo, PPF Plaza mjini
Mtwara
Rais akisalimiana na mmoja wa wajumbe a bodi ya wadhamini ya PPF, Bi. Amelye
Rais akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa uwekezaji, Steven Alfred
Kaimu Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Steven Alfred, akitoa hotuba
wakati wa uwekaji jiwe la msingi la jingo la kitegauchumi la Mfuko huo
mjini Mtwara Oktoba 10, 2015
Jengo la
kitegauchumi la ghorofa 5 linalomilikiwa na Mfuko wa Pensehni wa PPF,
eneo la Vigaeni mkoani Mtwara, ambalo Rais Jakaya Kikwete, ameliwekea
jiwe la msingi leo Oktoba 10, 2015
0 comments:
Post a Comment