SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) kwa ushirikiano na Azam Media Ltd, limezinduwa
rasmi michuano mipya ya soka nchini, Azam Sports Federation Cup.
Michuano
hiyo ambayo yaweza kufananishwa na mashindano ya baadhi ya nchi za
Ulaya na kwingineko kama vile FA Cup ya England na Copa del Rey ya
Hispania, itaendeshwa kwa mfumo wa mtoano na kushirikisha timu
mbalimbali si tu za Ligi Kuu ya Vodacom, bali pia nyingine kutoka
madaraja mengine mawili ya chini na kufanya idadi ya timu kuwa 64.
Mfumo
huu una msisimko wa aina yake huku ukitoa fursa kwa timu ya daraja la
chini kuitupa nje ya mashindano timu ya daraja la juu au maarufu. Azam Media imepata haki ya udhamini pamoja na matangazo ya shindano hili muhimu kwa kipindi cha miaka minne.
Ratiba ya mzunguko wa kwanza ambayo itaanza jumapili ya tarehe 8 mwezi huu wa kumi na moja ambayo litakuwa na timu 32 ambazo kati yake 24 zinatoka daraja la pili na zilizo bakia zikiwa zinatoka daraja la kwanza. Mizunguko ya shindano hili imepangwa katika tarehe ambazo hakuna michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom ili kuwawezesha mashabiki wa kandanda kufaidi uhondo wa mchezo huu kwa kipindi chote cha mwaka. Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington amezungumzia uzinduzi huo: “Huu ni wakati muhimu kwa wapenzi wa kandanda hapa Tanzania na pia ni mapinduzi ya matangazo ya luninga. Nimekuwa nikisema mara zote kuwa lengo letu ni kuufanya mchezo huu kuwa sehemu nzuri ya burudani kuliko shindano linalomalizika ndani ya muda mfupi.” Alipoulizwa kuhusu jina la shindano hilo amesema: “Limekuwa jambo zuri kuwa shindano hili jipya litabeba jina la chaneli yetu ya Azam Sports ambayo inatoa fursa kwa watazamaji kuona pia michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom, La Liga na sasa michezo ya ASFC moja kwa moja katika picha ang’avu zaidi. Pamoja na makubaliano ya karibuni ya kuwa mshirika rasmi wa TFF kwa matangazo ya michezo ya kimataifa ambayo wana haki, hatua hii inaimarisha uhusiano wa pande mbili hizi kwa manufaa ya michezo hapa Tanzania”. Mashindano haya yameipa fursa Tanzania kuweza kuwa na aina yake ya kombe la FA na kupitia Azam media swala hili lime hitimu. Vilevile Azam media imeweza pata fursa ya kuburudisha jamii ama wateja wake na kuwahakikishia kuwa Azam media ni kampuni ya nyumbani inayo lenga kuburudisha jamii haswa kwa wale wapenzi wa kandanda, kwani chezo huu umekuwa ni sisimko kubwa ndani ya Tanzania.

0 comments:
Post a Comment