https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Bomoabomoa yaendelea Dar, unawezaje kukwepa nyumba yako isibomolewe? majibu yako hapa… (+PICHAZ)

    Zoezi la kubomoa nyumba na majengo yaliyoingia ndani ya hifadhi ya miundombinu ya bomba la maji kutoka Ruvu Chini, limeendelea mwishoni mwa wiki ambapo baaadhi ya nyumba zilizokuwa zimejengwa ndani ya maeneo hayo ya Salasala zimevunjwa.
    01 copy
    Katapila likiwa ndani ya gari tayari kwa kazi ya bomobomoa eneo la Salasala ,Dar es salaam 
    Watu wengi wamekuwa hawaelewi vigezo vinavyozingatiwa hususani umbali sahihi wa mtu kujenga nyumba yake, hapa Mkurugenzi wa usimamizi na ufundi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka Dar es Salaam (DAWASA), Romanus Mwang’ingo  anaeleza>>
    Umbali sahihi unaopaswa wakazi hao kujenga makazi yao kutoka lilipo bomba la maji ni mita 15 kila upande ambapo hatua hiyo inapelekea kuwa jumla ya mita 30 ya umbali unaotakiwa
    ili kuhakikisha kunakuwepo na usalama na kuruhusu matengenezo mengine tofauti na hali ya awali ambayo huwezi hata kufanya kazi maana bomba limepita ndani ya uzio na makazi ya watu ambayo ni hatari kwa usalama wa maisha yao na mali zao”;-Romanus Mwang’ingo
    Maeneo yaliyohusishwa na ubomoaji huo ni pamoja na Bunju, Bondeni, Boko, Tegeta, Mbezi Intacheki, na Mbezi Tangibovu ili kuruhusu kukamilisha ujenzi wa bomba hilo la maji kutoka Ruvu Chini hadi Dar es salaam.
    02 copy
    09 copy
    Baadhi ya wakazi wa eneo la Salasala, Dar es salaam wakishuhudia zoezi la bomoabomoa
    10 copy
    Mafundi wakiendelea kubomoa nyumba iliyopo Salasala ili kupisha ujenzi
    03 copy
    04 copy
    05 copy
    .
    06 copy
    07 copy
    08 copy
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Bomoabomoa yaendelea Dar, unawezaje kukwepa nyumba yako isibomolewe? majibu yako hapa… (+PICHAZ) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top