KAMPUNI ya Jamii Media, ambao ni wamiliki wa mitandao maarufu ya mijadala kwa jamii kupitia mitandao ya jamii,JamiiForums na FikraPevu
nchini Tanzania, imelaani kitendo cha baadhi ya kundi/watu
walioishambulia miundombinu ya kampuni hiyo na kuzuia kupatikana kwa
huduma zake kwa siku kadhaa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo ndg Maxence Melo, tangu katikati ya mwezi Oktoba, 2015 mtandao wao pendwa wa JamiiForums ulianza kupata mashambulizi yaliyojulikana kama "DDOS Attack" mfululizo bila kikomo.
Amesema kwa kawaida yapo madaraja matatu tofauti ya mashambuzili (daraja la 3, la nne na la 7), na hivyo walipambana na mashambulizi kuanzia la daraja la tatu na la nne lakini waliokuwa wanataka kuhujumu miundombinu hiyo waligundua kuwa mashambulizi yao yamedhibitiwa, wakaamua kushambulia hadi daraja la 7 ambalo ndilo kubwa na la mwisho.
Muonekano wa picha unavyoonyesha jinsi miundombinu ya mtando huo ilivyoshambuliwa hadi kufikia Novemba mosi mwaka huu
Aidha, amesema mashambulizi ya DDOS Attack yanalenga kuzuia upatikanaji wa huduma na kufanya tovuti yeyeto husuani ya mtandao wa JamiiForums kuzidiwa (kuchelewa kufunguka) na kutoa huduma kwa watumiaji.
?Walipoona tumeweza kudhibiti daraja la nne, walishambulia daraja la saba, sasa makampuni mengi yanayotoa huduma za kusimamia mtandao 'Server Hosting Providers'yanapoona unashambuliwa sana yanakufukuza kwa kuwa wewe unashambuliwa na kuvuruga miundombinu yao? alieleza.
Amesema licha ya kampuni nyingi za kutoa huduma ya vihifadhi mtandao (Web Servers) kuogopa daraja la 7, yapo baadhi ya makampuni yanayoweza kukabiliana na hali hiyo.
"Hakuna mtoa huduma ambaye anakubali kuendelea kutoa huduma ya kuendelea kushikilia seva yako kama unaendelea kupata mashambulizi ya aina hii.
Picha hizi zinazoonyesha jinsi miundombinu ya mtando huo ilivyoshambuliwa hadi kufikia Oktoba 31, 2015
?Kilichotokea, siku ya uchaguzi tulishambuliwa lengo likiwa ni kuzuia watu wasiweze kupata taarifa kwa wale wanaoitembelea tovuti yetu na sisi baada ya kuona wamefanya hivyo tuligeukia upande wa pili wa Tovuti ya FikraPevu.com ambayo iko kwa ajili ya uandishi, tulivyoanza kuweka matokeo ya awali siku ya uchaguzi ili yaende kule kwa watu wanaofuatilia matokeo nchi nzima, tukaanza kushambuliwa huko pia? alikaririwa naFikraPevu.
"Tuliongeza hali ya usalama baada ya shambulizi la kwanza lakini walitushambulia tena Novemba 1, ambapo mashambulizi yalikuwa makubwa tena. Kuna Watetezi wa Haki za Binadamu ambao baada ya kujua tatizo letu walituunga mkono kiufundi ili kuhakikisha kuwa kila kinachotokea kitazuiwa na hata kabla hakijatokea. Wametushambulia kiufundi na sisi tumewadhibiti kiufundi na huduma zimerejea" aliongeza.
Soma zaidi =>JamiiForums, FikraPevu walaani nguvu inayotumika kuzuia uhuru wa maoni

0 comments:
Post a Comment