https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    JESHI LA POLISI LAPIGA " STOP "MAANDAMANO YA CHADEMA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU 2015 YALIYOTANGAZWA NA TUME...CHADEMA WASEMA MAANDAMANO KESHO YAKO PALE PALE


    Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
    Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa maandamano yao yako pale pale pamoja na kwamba polisi wamezuia-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

    Ofisi za Chadema wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo ndiyo maandamano ya Chadema yataanzia kesho Novemba 03,2015-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

    Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa vyombo vya habari
    Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limezuia maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) yaliyopangwa kufanyika Kesho Novemba 03,2015 katika mji wa Shinyanga kwa lengo la kupinga matokeo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015.
    Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha amesema wamezuia maandamano yaliyopangwa na Chadema kufanyika Novemba 03,2015 asubuhi akidai kuwa katika kipindi hiki hawaruhusu kufanyika kwa maandamano na mikutano kwa sababu jeshi la polisi limejikita katika kuangalia hali ya usalama utawale ili kusubiria kuapishwa kwa rais mteule na wabunge.
    Amesema pia wamezuia mikusanyiko yoyote isiyo rasmi ambayo inaweza kuleta uchochezi na uvunjifu wa amani kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria.
    Kamanda Kamugisha amesema Chadema wametoa taarifa kuwa Kesho wanataka kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25,2015 na baada ya kufanya maandamaano hayo wanataka kutoa ujumbe kwa serikali.
    Amewashauri wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga wasishawishiwe na viongozi wa vyama vya siasa,na kuwaomba wabaki majumbani,waendelee na shughuli zao na kutokubali kurubuniwa au kushawishiwa kuandamana kwani wanaowashawishi hawatakuwa mbele .
    Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama amesema hawajapata taarifa wala maelekezo yoyote kuhusu kuzuiwa kwa maandamano yao na wanaendelea kujiandaa na wanachama wao kwa maandamano kama walivyopewa maagizo na viongozi wao wa kitaifa.
    Amesema kesho 03.11.2015,watafanya maandamano ya amani kuanzia ofisi za Chadema wilaya kisha kuzunguka mji mzima wa Shinyanga kuanzia saa tatu asubuhi kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume,na kwamba ni maandamano ya nchi nzima siyo Shinyanga pekee.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JESHI LA POLISI LAPIGA " STOP "MAANDAMANO YA CHADEMA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU 2015 YALIYOTANGAZWA NA TUME...CHADEMA WASEMA MAANDAMANO KESHO YAKO PALE PALE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top