Kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Brazil Ramires bado anaamini kwamba kocha wa klabu yake Jose Mourinho bado ana sapoti kubwa kutoka kwa wachezaji wa Chelsea licha ya timu yao kupoteza michezo sita ya ligi mpaka sasa, ikijumlishwa na kipigo kutoka kwa Liverpool cha mabao 3-1 Jumapili iliyopita.
Ramires alifunga goli la kuongoza dhidi ya Liverpool lakini magoli mawili kutoka kwa Philippe Coutinho na moja kutoka kwa Christian Benteke yalipeleka msimba mzito kwa Wabluu hao wa London.
Chelsea wanashika nafasi ya 15 baada ya kupoteza michezo sita katika michezo 11 waliyocheza.
Mourinho yuko kwenye presha kubwa hivi sasa baada ya matokeo mabovu mfululizo kwa timu yake.
Licha ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu juu ya mustakabali wa kocha wao, Ramires amesisitiza kuwa kuna sapoti kubwa sana ya wachezaji kwa kocha wao.
Aliiambia tovuti ya Chelsea kuwa: “Tunajitahidi sana kumsaidia yeye (Mourinho) pindi tuwapo uwanjani, imeshindikana kufanya hivyo Jumapili iliyopita lakini bado tunajaribu kwa kila namna kushinda kila mchezo, hili ni kundi hivyo tukishindwa basi, Jose anatakuwa ameshindwa pia, sote tuko pamoja”.
“Tunahitaji kucheza kama ambavyo tulivyokuwa tukicheza hapo awali na kushinda michezo mingi”.
Kwa upande wake, Oscar amewasisitiza wenzake kujituma kwa kadri wawezavyo huku akikiri kuwa hali si shwari kunako klabu yao ama kwa kocha wao au kwa wachezaji wenyewe.
Aliongeza: “Liverpool walicheza vizuri sana katika kipindi cha pili kuliko sisi. Coutinho alicheza vizuri, tulijaribu kila iwezekanavo lakini ilishindikana. Tunahitaji kukaza buti tu..”
“Kila mtu hapa anajitahidi kumsaidia lakini hali si shwari kwa Jose, wachezaji na mashabiki pia, lakini inatupasa tuanze kushinda tena”.
Ramires akishangilia goli lake la kwanza katika mchezo dhidi ya Liverpool
Christian Benteke (wa pili kushoto) akiifungia goli la tatu Liverpool dhidi ya Chelsea
Mourinho akijadiliana jambo na jopo lake
0 comments:
Post a Comment