Mabao yaliyoirejesha Norwich ligi kuu England yaliwekwa kimiani na Cameron Jerome pamoja na Nathan Remond.
Katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Wembley, mbali ya kukabidhiwa kombe, pia Norwich wameondoka na jumla ya paundi millioni 130 .
Mashabiki wa Norwich wakiwa na furaha baada ya timu yao kuifunga Middlesbrough mabao 2-0 na kufanikiwa kurejea ligi kuu England msimu ujao.