Mhubiri
maarufu duniani TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini
Nigeria ametua jijini Dar es salaam leo tayari kwa kushuhudia
kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya
Alhamisi.
Mara
tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB
Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho
Kikwete kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru
na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua
amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake,
akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka
tele katika awamu hii mpya.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church
of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
TB Joshua ametua jijini Dar es salaam tayari kwa kushuhudia kuapishwa
kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhubiri TB Joshua wa kanisa la
Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni
hii.
Picha na Freddy Maro
0 comments:
Post a Comment