Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.
“
Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa
hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala
kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za
uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa
muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali
za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta
huduma huko”. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :
Rais
amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ilishamaliza
muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya
Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.
Dkt.
Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine.
Balozi
Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya
wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote
za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na
kuhudumia wananchi kama ipasavyo.
Tayari
Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na
kulipa madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.
Hata
hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini
zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha
mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular
Maintenance).
Balozi
Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote
katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi
za umma zinatekelezwa ipasavyo.
“Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao” Amesisitiza Balozi Sefue.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment