Headlines zimerudi China..mamlaka ya
hali ya hewa imetoa tahadhari kwa watu kutoka nje baada ya kutokea
uchafuzi wa mazingira ulioukumba mji mkuu wa nchini hiyo Beijing.
Mji huo ambao umekuwa katika hali ya
tahadhari tangu mwanzoni mwa mwaka huu unasemekana kukumbwa na wingu
zito baada ya mkaa kuwashwa maeneo mbalimbali kukabiliana na baridi
kali.
Serikali ya China imetoa amri ya
kutotoka nje kwa mamilioni ya watu kwa nia ya kupunguza madhara hayo
kwao kwa muda wa siku tatu tangu jana jumapili na hali hiyo inatarajiwa
kuendelea hadi siku ya Jumatano.
Viwango vya uchafuzi katika mji huo ni mara 17 zaidi ya viwango vya usalama vinavyotolewa na shirika la afya duniani WHO.
0 comments:
Post a Comment