Serikali
imefuta hatimiliki ya shamba la mkonge la Kikwetu, mkoani Lindi baada
ya mmiliki wake kampuni ya Amboni Estates Ltd, kushindwa kuliendeleza.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi
wa manispaa hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa
Ilulu mjini hapa juzi.
Shamba
hilo linalodaiwa kupewa hati ya umiliki wa miaka 99 na baadaye kampuni
ya Tasco kabla ya kuchukuliwa na Mohamed Enterprieses Tanzania Ltd
lilikuwa likizalisha mkonge kwa ajili ya kutengeneza magunia na bidhaa
zingine.
Akizungumza
katika mkutano huo, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kupitia mamlaka
aliyopewa kisheria, Rais Magufuli amefuta leseni ya umiliki wa shamba
hilo na kuwa chini ya serikali.
Majaliwa
alisema tayari shamba hilo lipo huru na kampuni ya BSG ipo huru kujenga
mitambo itakayotumika kusafishia gesi asilia kwenye eneo hilo.
Kuhusu
uendelezwaji wa kiwanda cha kuzalisha saruji cha Meis ambacho ujenzi
wake umesimama kwa muda kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za
kisiasa, Majaliwa alisema kazi hiyo inatarajiwa kuanza tena muda mfupi
ujao baada ya kupatikana kwa wataalam.
Alisema
kujengwa kwa viwanda ndani ya mji huo, kutasaidia kupunguza tatizo la
upatikanaji wa ajira kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi na vitongoji vyake.
Shamba
la mkonge la Kikwetu lililopo ndani ya Manispaa ya Lindi awali lilikuwa
linamilikiwa na kampuni ya Amboni Estates Ltd halafu Tasco na baadaye
Mohamed Enterprieses Tanzania Ltd ya jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment