https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI AFANYA ZIARA TRL

    mp2 
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofanya ziara katika Shirika la Reli Tanzania (TRL)ili kuhakikisha ufanyaji kazi wa shirika hilo linaendana na kasi yaRais wa awamu ya tano Mh. John Pombe Magufuli.
    mp4
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka akikagua maeneo mbalimbali wakati alipofanya ziara katika Shirika la Reli Tanzania (TRL).
    MP5
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjakaakikagua karakana ya Shirika la Reli Tanzania (TRL)wakati alipotembelea shirika hilo leo.

     

                                                                                Na Ally Daud-Maelezo
                                                                                                   Dsm
     

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shabani Mwinjaka amefanya ziara katika Shirika la Reli Tanzania (TRL)ili kuhakikisha ufanyaji kazi wa shirika hilo linaendana na kasi yaRais wa awamu ya tano Mh. John Pombe Magufuli.
    Katika ziara hiyo Bw. Mwinjaka alikagua karakana za shirika hilo ili kuona utendaji wake na kusisitiza ukarabati wa mebehewa yaliyobaki kumaliziwa ndani ya siku 30.

    Hata hivyo katibu huyo amestushwa na habari ya kuanguka kwa mabehewa 50 ya mafuta yaliyokuwa yanajaribiwa huko Tanga.
     

    “Nimestushwa na taarifa ya kuanguka kwa mabehewa 50 ya mafuta katika majaribio baada ya kujazwa maji ,yangekuwa yana mafuta ingekua hasara kubwa kwa Tanzania hivyo nataka tatizo hilo lishughulikiwe haraka iwezekanavyo kunusuru mabehewa yaliyobaki .”alisema Mwinjaka
    Mbali na hayo Bw.Mwinjaka alisema kwamba reli ambazo zimehifadhiwa katika karakana hizo ziondolewe na zikamalizie ujenzi wa reli ambazo hazijaisha kuliko kukaa bila ya matumizi huku kukiwa na shida ya mataaluma hayo.

    Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Bw.Elias Mshana amesema kwamba wapo katika mchakato wa kumalizizia ukarabati wa mabehewa yaliyobaki pamoja na marekebisho ya reli zilizoharibika na mpaka 31 Desemba mwaka huu zitakua zimetengemaa.

    “Tunatarajia mpaka tarehe 31 Decemba mwaka huu tutakua tumemaliza kukarabati mabehewa na reli zilizoharibika ili zianze kutumiwa rasmi ili kuleta maendeleo katika Nchi” Alisema Bw. Mshana.
    You might also like:
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI AFANYA ZIARA TRL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top