TIMU
ya VfL Wolfsburg imeitupa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
Manchester United baada ya kuichapa mabao 3-2 katika mchezo wa Kundi B
Uwanja wa Volkswagen Arena usiku wa kuamkia leo.
Wolfsburg
inamaliza na pointi 12, ikifuatiwa na PSV pointi 10, wakati United
inabaki na pointi zake nane- hivyo inahamia kwenye michuano ya Europa
League.
Mbaya
wa United alikuwa ni Ronaldo Aparecido Rodrigues aliyefunga mabao
mawili jana dakika ya 13 na 84, wakati bao lingine la wenyeji limefungwa
na Adelino Andre Vieira de Freitas dakika ya 29.
Mabao
ya United yamefungwa na Anthony Martial ambalo lilikuwa la kwanza
mchezoni dakika ya 10, wakati lingine Wolfsburg walijifunga kupitia kwa
Josuha Guilavogui dakika ya 82.
Kipa wa United, David De Gea akiwa hoi baada ya mchezaji mwenzake, kushindwa kumzuia Naldo kuifungia Wolfsburg bao la ushindi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mchezo mwingine wa kundi hilo, PSV imeshinda 2-1 dhidi ya CSKA Moscow mabao yake yakifungwa na Luuk de Jong dakika ya 78 na Davy Propper dakika ya 85, huku la wageni likifungwa na Sergei Ignashevitch kwa penalti dakika ya 76 Uwanja wa Philips. Real Madrid imefanya ‘unyama’ ikishinda 8-0 dhidi ya Malmo FF katika mchezo wa Kundi A, Cristiano Ronaldo peke yake akifunga manne, Karim Benzema mawili na moja Mateo Kovacic Uwanja wa Santiago Bernabeu. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Paris Saint-Germain imeichapa 2-0 Shakhtar Donetsk mabao ya Lucas Rodrigues Moura da Silva dakika ya 57 na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 86 Uwanja wa Parc des Princes. Real inamaliza na pointi 16, ikifuatiwa na PSG 13, wakati Shakhtar iliyovuna pointi tatu tu nayo inakwenda Europa League.
Manchester
City imeshinda 4-2 dhidi ya Borussia Monchengladbach katika mchezo wa
Kundi D Uwanja wa Etihad, Raheem Sterling akifunga mabao mawili dakika
ya 79 na 81, mengine David Silva dakika ya 16 na Wilfried Bony dakika ya
85, huku ya wageni yakifungwa na Julian Korb dakika ya 19 na Raffael
Caetano de Araujo dakika ya 42.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Sevilla imeichapa bao 1-0 Juventus, mfungaji Fernando Llorente dakika ya 65 Uwanja wa Ramon-Sanchez Pizjuan.
Man City inamaliza na pointi 12, ikifuatiwa na Juve 11, wakati Sevilla yenye pointi sita inahamia Europa League.
Raheem Sterling akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Manchester City PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Atletico Madrid imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Benfica katika mchezo wa Kundi C, mabao yake yakitiwa kimiani na Saul Niguez dakika ya 33 na Luciano Vietto dakika ya 55, kabla ya Kostas Mitroglou kuwafungia wenyeji la kufutia machozi dakika ya 75 Uwanja wa Luz. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Galatasaray imetoa sare ya 1-1 na FC Astana bao lake likifungwa na Selcuk Inan dakika ya 64 na wageni likifungwa na Patrick Twumasi dakika ya 62 Uwanja wa Turk Telekom Arena. Atletico inamaliza na pointi 13, ikifuatiwa na Benfica pointi 10, wakati Galatasaray iliyomaliza na pointi tano, inahamia Europa League.
Michuano
hiyo inaendelea leo, Arsenal watakuwa wageni wa Olympiakos katika
mchezo wa Kundi F Uwanja wa Georgios Karaiskakis wakihitaji lazima
kushinda ili kwenda hatua ya mtoano.
Kwa sasa Arsenal ina pointi sita katika nafasi ya tatu, nyuma ya Olympiakos wenye pointi tisa na Bayern Munich pointi 12.
Chelsea watakuwa
wenyeji wa FC Porto Uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo ambao The
Blues watahitaji japo sare tu kujihakikishia kusonga mbele.
Mechi
nyingine za leo ni kati ya Valencia CF na Lyon, Roma na BATE Borisov,
KAA Gent na Zenit St Petersburg, Dynamo Kyiv na Maccabi Tel Aviv na Kiev
Olympic, Dinamo Zagreb na Bayern Munich na Bayer 04 Leverkusen na Barcelona.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, PSV imeshinda 2-1 dhidi ya CSKA Moscow mabao yake yakifungwa na Luuk de Jong dakika ya 78 na Davy Propper dakika ya 85, huku la wageni likifungwa na Sergei Ignashevitch kwa penalti dakika ya 76 Uwanja wa Philips. Real Madrid imefanya ‘unyama’ ikishinda 8-0 dhidi ya Malmo FF katika mchezo wa Kundi A, Cristiano Ronaldo peke yake akifunga manne, Karim Benzema mawili na moja Mateo Kovacic Uwanja wa Santiago Bernabeu. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Paris Saint-Germain imeichapa 2-0 Shakhtar Donetsk mabao ya Lucas Rodrigues Moura da Silva dakika ya 57 na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 86 Uwanja wa Parc des Princes. Real inamaliza na pointi 16, ikifuatiwa na PSG 13, wakati Shakhtar iliyovuna pointi tatu tu nayo inakwenda Europa League.
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid mabao manne katika ushindi wa 8-0 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Atletico Madrid imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Benfica katika mchezo wa Kundi C, mabao yake yakitiwa kimiani na Saul Niguez dakika ya 33 na Luciano Vietto dakika ya 55, kabla ya Kostas Mitroglou kuwafungia wenyeji la kufutia machozi dakika ya 75 Uwanja wa Luz. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Galatasaray imetoa sare ya 1-1 na FC Astana bao lake likifungwa na Selcuk Inan dakika ya 64 na wageni likifungwa na Patrick Twumasi dakika ya 62 Uwanja wa Turk Telekom Arena. Atletico inamaliza na pointi 13, ikifuatiwa na Benfica pointi 10, wakati Galatasaray iliyomaliza na pointi tano, inahamia Europa League.
Kocha
Arsene Wenger akimnyooshea kidole Olivier Giroud wakati wawili hao
wanazungumza kwenye mazoezi ya timu hiyo jana asubuhi kabla ya mchezo
wao wa leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment