Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kwa waandishi wa habari, ripoti
Bandari ya Dar es salaam iliyobaini mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya
Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana.
Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Kuvunjwa
kwa bodi hiyo kunatokana na utendaji mbovu wa Mamlaka hiyo kwa muda
mrefu na kitendo cha kutokuchukua hatua katika vyanzo husika.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo, Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kutenguliwa kwa uteuzi huo kunatokana na
ziara alizofanya katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini uwepo wa
mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati
ya Machi na Septemba mwaka jana.
Amesema
upotevu huo unatokana na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo ambao
unatoa mwanya wa kupoteza mapato ya serikali na kutaka mfumo huo
ubadilishe kufikia Desemba 11.
Waziri
Mkuu, Majaliwa amesema kuwa kutokana na utendaji wa bandari huo mbovu,
ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji wa makontena hayo na bila ya
kuwepo kwa taarifa yeyote, hivyo amewasimamisha kazi wasimamizi 8 wa
Bandari Kavu (ICD) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari
Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante
pamoja na James Kamwomwa.
Wengine
ambao hakuwemo kwenye ripoti hiyo ambao ni viongozi wa sekta zilizotoa
ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari lakini ni wahusika wakuu ambao
ni Shaban Mngazija Aliyekuwa Meneja Mapato, Rajab Mdoe Mkurugenzi wa
Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu, Ibin Masoud Kaimu Mkurugenzi wa Fedha
,Apolonia Mosha Meneja wa Bandari Msaidizi (Fedha).
Waziri
Mkuu, amesema kuwa katika ziara yake kwa Shirika la Reli Nchini (TRL)
alibaini matumizi mabaya ya fedha ya Sh.Bilioni 13 nje ya utaratibu
ambao uchunguzi unakamilishwa kwa waliohusika.
0 comments:
Post a Comment