Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo, Mbwana Samatta.
BAADA ya
kushinda Tuzo ya Afrika kama Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji
wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo,
Mbwana Samatta anatarajiwa kupongezwa na kuagwa rasmi na mashabiki wake
leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem
jijini Dar.
Akizungumza na Uwazi, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mapema kabla ya saa kumi na mbili jioni kutakuwa na matembezi sambamba na Samatta maeneo ya Temeke na baada ya hapo, saa kumi na mbili atatinga ndani ya Dar Live kuwaaga mashabiki wake.
“Kutakuwa
na red carpet ambapo mashabiki wote watapata fursa ya kupiga picha na
Samatta sambamba na kuzungumza naye mawili matatu kisha burudani kabambe
itafuatiwa kutoka kwa Khalid Chokoraa ambaye tayari amemtungia wimbo,
Twanga Pepeta chini ya Ali Chocky pamoja na Msagasumu,” alisema Mbizo na
kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni 5,000 kwa wote.
Y
0 comments:
Post a Comment