WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA WILAYA YA MISUNGWI, ACHANGIA MIRADI YA MAENDELEO
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na Wakuu wa Idara wa
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza mara baada ya kupokelewa
wilayani hapo. Waziri Kitwanga aliwataka viongozi hao kuongeza nguvu
kubwa ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na si
kuwasumbua wafanyabiashara wadogowadogo. Pia aliwataka viongozi hao
wahakikishe hakuna mwanafunzi atakayekaa chini darasani ifikapo mwakani.
Picha zote na Felix Mwagara.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akiwauliza maswali viongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakati alipokuwa
anakagua ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Aimee Milembe
wilayani humo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akiwauliza maswali viongozi wa Kata ya
Mabuki wilayani Misungwi wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa Kituo cha
Afya cha Kijiji cha Mhungwe katika kata hiyo. Waziri Kitwanga alichanga
milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hicho cha afya. Wapili kulia
ni Diwani wa Kata hiyo, Nicodemus Ihano, na wapili kushoto ni Mtendaji
wa Kata hiyo, Angelina Nyanda.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kushoto) akiangalia ufa katika moja ya
madarasa ya Shule ya Msingi Lubuga iliyopo Kata ya Mabuki wilayani
Misungwi. Waziri Kitwanga aliagiza darasa hilo livunjwe na ameahidi
kuchangia matofali pamoja na mifuko ya saruji...
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Diwani wa Kata ya
Misungwi, Mwamba Makune, wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika
Shule ya Sekondari ya Aimee Milembe jimboni humo kwa ajili ya ukaguzi wa
miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na viongozi wa Serikali ya
vijiji katika Kata ya Misungwi.
Mkuu
wa Wilaya ya Misungwi, Mwajuma Nyiruka akizungumza na Wakuu wa Idara wa
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi (hawapo pichani) kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
(kushoto) ili azungumze na wakuu hao wa idara. Waziri Kitwanga aliwataka
viongozi hao waongeze nguvu ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wenye
mitaji mikubwa na si kuwasumbua wafanyabiashara wadogowadogo. Pia
aliwataka viongozi hao wahakikishe hakuna mwanafunzi atakayekaa chini
darasani jimboni humo ifikapo mwakani. Kulia ni Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo, Nathan Mshana. Picha zote na Felix Mwagara.
0 comments:
Post a Comment