Wachezaji wa Simba wakishangilia moja ya magoli yao yalifungwa kwenye mchezo wa leo dhidi ya African Sports
Klabu ya
Simba imeendelea kuzikimbiza Yanga na Azam katika mbio za kuwania
ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu baada ya
kufanikiwa kuichapa African Sports kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza
wa raundi ya pili ya ligi hiyo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Hamisi
Kiiza ameibuka shujaa wa mchezo huo akifanikiwa kuweka bao mbili kambani
ndani ya kipindi cha kwanza huku bao la tatu ndani ya kipindi cha
kwanza likifungwa na Hasan Kessy.Beki wa African Sports (kushoto) akimdhibiti Ibrahim Ajib wakati wa mchezo wa Simba vs African Sports
Bao la ushindi la mnyama wa Msimbazi limekwamishwa wavuni na Haji Ugando na kukamilisha kalamu ya mabao kwa siku ya leo.
Matumaini
ya Simba kuibuka kidedea kwa kutwaa ndoo ya ligi msimu huu yameibuka
baada ya mtani wao Yanga kukwama jijini Tanga mbele ya Coastal Union kwa
kipigo cha bao 2-0. Azam ambao leo wangecheza na Tanzania Prisons
hawapo nchini hivyo mchezo huo umeahirishwa hadi hapo watakaporejea
nchini.Haji Ugando akijaribu kumtoka Ally Ahmed wa African Sports
Yanga
bado wanaongoza ligi wakiwa na pointi 36, Azam wako nafasi ya pili kwa
pointi 36 sawa na Yanga lakini wao wanafaida ya mchezo mmoja mkononi
ambao walitakiwa wacheze leo.Raia wa kigeni waliovalia jezi nyekundu pia walikuwa wakishuhudia pambano kati ya Simba dhidi ya African Sports
Matokeo
hayo yanaiingiza Simba kwenye orodha ya timu ambazo zinawania ubingwa
msimu huu kutokana na tofauti ya pointi lakini bado kuna mechi nyingi
ambazo zinaweza zikaamua nani ataibuka bingwa wa msimu huu.Ibrahim Ajib akichuana na Juma Shemvuni
Jackson
Mayanja ambaye anashikilia nafasi ya kocha mkuu kwa muda tangu
kutimuliwa kwa Dylan Kerr ameendelea kufurahia ushindi ndani ya klabu
hiyo kwani ameshinda mechi zote ambazo ameingoza Simba.
Mayanja
ameingoza Simba kwenye mechi tatu za ligi (Simba vs Mtibwa Sugar, Simba
vs JKT Ruvu na Simba vs African Sports) na kuvuna ponti tisa katika
michezo hiyo lakini paia alikiongoza kikosi hicho kwenye ushindi wa
magoli 3-0 kwenye kombe la FA dhidi ya Burkina Faso ya mkoani Morogoro.Mashabiki wa Simba wakiishanglia timu yao
0 comments:
Post a Comment