WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu,
mara baada ya kuapishwa Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
Ametoa
pongezi hizo wakati Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakiwa wametia
saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi
wa habari.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi hao, kuwa waaminifu, kuwajibika na kutoa taarifa ya utendaji kwa wananchi.
Aidha,
alisema kuwa, viongozi wengine watakao apa mbele ya Kamishna wa Tume ya
Maadili ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa
Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali kudhibiti na kufuatilia
matumizi ya rasilimali fedha.
“Wakuu wa Wilaya watahakikisha fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike katika shughuli zilizokusudiwa” alisema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya
Awamu ya Tano, kwakuwa itatimiza ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais na
Makamu wa Rais walizitoa wakati wa Kampeni.
Makatibu
Wakuu na Naibu Katibu Wakuu hao, wameapishwa na Mheshimiwa Rais Dkt.
John Magufuli, ambapo shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais
Mheshimiwa Samia Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke
wa Mheshimiwa Rais mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI
S.L.P 3021
1141O DAR ES SALAAM
IJUMAA, JANUARI 1, 2016.
0 comments:
Post a Comment