https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    JE, MWISHO WA CHELSEA LIGI YA MABINGWA UMEISHIA PARIS?

    PSG-Chelsea
    Na Muba Seif
    Juzi tarehe 16/02/2016 Chelsea ilikuwa ugenini ikiivaa PSG kwenye uwanja wake wa nyumbani ‘Parc des Princes’ ikiwa mbele ya mashabiki wao wapatao 70,000.
    PSG tunayoizungumzia hapa ni ile ambayo imesheheni wachezaji karibu wote wenye majina makubwa kabisa barani Ulaya wakiongozwa na Zlatan Ibrahimovic, Di Maria, Thiago Silva na David Luiz.
    Lakini Chelsea huku ikicheza kwa umakini mkubwa iliambula kipigo cha mabao 2-1. Pengine swali kubwa ambalo watu wanajiuliza ni je Chelsea itaweza kutoka kifua mbele katika mechi ya marudiano inayotarajiwa kupigwa wiki tatu zijazo?
    Kwanza tukiangalia mechi yenyewe iliyopigwa pale Ufaransa, Chelsea walicheza kitimu zaidi kuanzia golikipa, mabeki, viungo na washabuliaji.
    Ilipolazimika kushambulia kama timu ilishambulia kwa pamoja lakini pia walipolazimika kukaba kama timu walikaba kwa pamoja, hivyo kuwapa PSG wakati mgumu sana wa kuipenya ngome yao ambayo ilikuwa inalindwa kati na mabeki ambao hawajazoeana kufanyakazi pamoja pale katika beki ya kati (Branislav Ivanovic na Gary Cahil). Pamoja na kwamba walikuja kuruhusu goli la Edson Cavan dakikaya 78, bado mabeki hawa wawili wa kati walifanya kazi kubwa sana na nzuri dhidi ya washambuliaji hatari wa PSG pale mbeleyagoli.
    Pamoja na kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa John Terry atakuwa amerudi mechi ya marudiano bado mabeki hawa wawili watakuwa washazoeana kufanyakazi pamoja kama mabeki wa kati na hivyo watakuwa bora na wagumu zaidi dhidi ya washambualiaji wa PSG.
    Chelsea walicheza zaidi mchezo wa kuvamia ghafla ‘counter attack’ ambao kama washambuliaji wangekuwa na umakini kidogo basi hadithi ingebadilika na wala swali la kwamba je huu ni mwisho wa Chelsea lisingekuwepo.
    Chelsea pamoja nakupata nafasi kadhaa lakini nafasi ambayo watakuwa wanaikumbuka sana ni nafasi ya Diego Costa, pale kipa wa PSG alipouparua kidogo kwa vidole mpira wa kichwa wa mshambuliaji huyo aliyerejea katika ubora wake.
    Bado nina amini kama ule mpira wa kichwa wa Diego Costa ungeingia kambani basi ladha ya mechi ingebadilika sana, maana PSG wangeta kakushambulia zaidi kutafuta bao la kusawazisha, kitu ambacho kingekuwa ni hatari kwao maana Chelsea ina washambuliaji wa pembeni wanaokimbia sana na mipira ambao wangeweza kuwadhuru PSG kwa ‘Counter Attack’ kama vile Eden Hazard, Willian na Pedro.
    Kumbuka mechi ijayo watakuwa darajani ‘Stanford Bridge’ mbele ya mashabiki wapatao 40,000 itakuwa nadra sana kuacha kuzitumia nafasi kama ile ya Diego Costa mbele ya kelele za mashabiki wao pale uwanja wa nyumbani. Pia usisahau kwamba Chelsea watakuwa wanatafuta ushindi wabao 1-0 ili kupita, jambo ambalo naliona kama linawezekana pale darajani.
    PSG pia ikumbukwe walikuwa wanajiamini zaidi walipokuwa mbele ya mashabiki wao, lakini watakapokuwa Stamford Bridge kujiamini kule hakutakuwepo.
    Kwenye mashindano kama haya hasatimu zote zinapokuwa kubwa zenye wachezaji mahiri kama hizimbili, inakuwa ngumu kidogo watu wanapocheza ugenini kama tulivyoshuhudia kwa Chelsea juzi pale Ufaransa.
    Siku zote faida inakuwa kwa yule ambaye anamalizia mchezo wa mwisho nyumbani, kwa maaana atafanya kila linalowezekana kuhakikisha anapita katika hatua inayofata (ikumbukwe anayepita katika mechi hii anaingia robo fainali).

    Hivyo basi, ukichukulia mambo ya fuatayo; kwanza Chelsea wanagoli la ugenini, pili watakuwa wanacheza nyumbani mbele ya mashabiki wao, na tatu kiongozi wao uwanjani captain John Terry atakuwa amerudi kuja kutia nguvu beki ya kati, basi Chelsea wana nafasi kubwa ya kuwaondoa PSG na kutinga robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JE, MWISHO WA CHELSEA LIGI YA MABINGWA UMEISHIA PARIS? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top