February 20 Yanga itakuwa mwenyeji kwenye pambano la marejeano dhidi ya Simba baada ya timu hizo kukutana mara kwanza kwenye ligi msimu huu September 26 mwaka huu na Yanga kufanikiwa kuitandika Simba kwa bao 2-0.
Magoli ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba Amis Tambwe na nyota wa zamani wa Mgambo JKT Malimi Busungu ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitokea kwa maafande hao wa Kabuku wilaya ya Handeni, Tanga.
Kuelekea pambano la marudiano, nimekuandalia habari matukio kadhaa kupitia namba mbalimbali kutokana na msimamo wa ligi ulivyo hadi sasa.
- Nafasi zilipo Simba na Yanga kwenye msimamo wa ligi
Imecheza mechi 19
Imeshinda mechi 14, imetoka sare mara 3, imefungwa mechi 2
Yanga ipo nafasi ya pili inapointi 42
Imecheza mechi 18
Imeshinda mechi 13, imetoka sare mara 4, imefungwa mara 1
- Wachezaji wenye magoli mengi toka Simba na Yanga kwenye orodha ya wafungaji bora
Hamisi Kiiza magoli 16 ndiye kinara wa upachikaji mabao wa VPL hadi sasa
Ibrahim Ajib ana magoli 8, yeye anakamata nafasi ya pili kwa magoli mengi ndani ya Simba SC lakini kwenye ligi yupo nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji bora.
Yanga SC
Amis Tambwe magoli 14 anakamatia nafasi ya pili kwa ufungaji kwenye ligi nyuma ya Kiiza
Donald Ngoma ana magoli 10 anashika nafasi ya pili kwa ufungaji kwenye timu ya Yanga lakini yupo nafasi ya tatu kwenye ligi akilingana kwa magoli na Jeremia Juma Mgunda (TZ Prisons) .
- Magoli ya kufunga na kufungwa kati ya Simba na Yanga
Imefunga magoli 35
Imefungwa magoli 11
Tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa 24
Yanga
Imefunga magoli 42
Imefungwa magoli 9
Tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa 33
- Timu ambazo zimezifunga Simba na Yanga kwenye ligi msimu huu
Yanga imefungwa na Coastal Union January 30, 2016
- Umuhimu wa mechi ya February 20 kwa Simba na Yanga
Endapo ‘mnyama’ atashinda mchezo huo atafikisha pointi 48 na ataendelea kuongeza gap la pointi dhidi ya wapinzani wake wanaowania ubingwa wa VPL msimu huu Yanga na Azam.
Yanga
Watoto wa Jangwani wakifanikiwa kumkalisha mnyama kwa mara ya pili msimu huu, watafikisha pointi 46 na kurejea kilaleni mwa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Simba ambayo itasalia na pointi zake 45.
Sare
Mchezo huo ukimalizika kwa sare hiyo inamaanisha Simba itaendelea kubaki kileleni mwa ligi baada ya kugawana pointi mojamoja na Yanga.
0 comments:
Post a Comment