Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa amejikuta katika utata wa tukio la kumng'ata mchezaji wa Everton, wakati Romelu Lukaku akiyayusha ndoto za Chelsea za kutwaa kombe lolote msimu huu baada ya kufunga magoli mawili yaliyoitoa kwenye michuano ya kombe la FA.
Diego Costa alionekana akigusisha mdomo wake kwenye shingo ya mchezaji wa Everton Gareth Barry wakati walipokuwa wakigombana na kumpelekea Costa kupatiwa kadi nyekundu ya kwanza tangu ahamie kucheza nchini Uingereza.
Costa mwenyewe amekanusha kumg'ata Barry, na hata mwisho wa mchezo huo makocha wote wa timu hizo Guus Hiddink na Roberto Martinez walisita kutoa tuhuma kwa mshambuliaji Diego Costa.

0 comments:
Post a Comment