Radamel Falcao amesema kwamba hakupewa muda wa kutosha kuzoea mazingira ya Ligi ya England wakati yuko Manchester United chini ya kocha Louis Van Gaal.
Falcao amesema: “Nilipata wakati mgumu sana wakati nikiwa Manchester United. Kila mtu aliona namna kulivyokuwa hakuna utulivu, nilipewa muda mfupi sana wa kucheza.
“Ilikuwa ni kama hivi, leo napewa dakika 60, kesho 45, keshokutwa 20 hali hiyo inakufanya ukose utimamu na kujiamini, kwa sababu hujui hasa wapi utacheza na kwa wakati gani na kipi hasa kocha anahitaji kutoka kwako.
“Ulikuwa ni wakati mgumu sana. Nilikuwa nikipewa nafasi ya kuanza mara kwa mara mwanzoni wakati nikiwa Monaco, lakini baada ya kupata jeraha la goti wakati na baadaye kupona na kuja United ambako nilikuwa nikikutana na kocha mpya, wachezaji wapya, sikupewa fursa ya kutosha hata kidogo.”
Lakini hata hivyo Falcao amesema kuwa licha ya mambo yote hayo, hakuwahi kutofautiana kwa namana yoyote ile na kocha Louis Van Gaal.


0 comments:
Post a Comment