https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Hakuna klabu yoyote katika EPL Yenye magoli mengi kuzidi MSN msimu huu.

    ARSENAL walifundishwa somo lingine usiku wa jana katika darasa la uwanja wa Nou Camp na FC Barcelona – waliongozwa na MSN.
    BAR-V-ARS-main_2746552aLionel Messi, Luis Suarez na Neymar kama kawaida walikuwa kwenye orodha ya wafungaji – kwa mara nyingine tena – wakati viongozi hao wa La Liga wakifanikiwa kuvuka kwenda hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya.
    Wakatalunya waliitoa Gunners kwa ushindi wa jumla wa 5-1, wajumbe wa MSN pekee ndio waliofunga magoli hayo matano – Messi akifunga matatu, Neymar 1 na Suarez 1. Arsena vs MSNKikosi cha Arsene Wenger sio timu ya kwanza kukutana na kisago kilichosimamiwa na MSN, na itakuwa sio timu ya kwanza kukumbana dhahama ya vijana hao watatu wa KiAmerika ya kusini.
    02_17102046_5f6c34_2746583aMpaka kufikia sasa MSN wameshafunga magoli 106 msimu huu, yakiwemo magoli 68 katika La Liga pekee yake.
    Idadi hii ni kubwa kuliko timu yoyote katika ligi kuu ya England katika msimu huu.
    kane-vardy-e1448380217378Timu zinazoongoza kwa kufunga magoli mengi katika Premier League msimu huu ni  Leicester na Tottenham wakifunga magoli 53 — na kwa sasa ndio wanaongoza ligi kwa kushika nafasi ya kwanza na ya pili.

    Messi, Suarez na Neymar wamefunga magoli 68 pekee yao kwenye La Liga msimu huu.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hakuna klabu yoyote katika EPL Yenye magoli mengi kuzidi MSN msimu huu. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top