https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Ikulu Yakanusha Taarifa Ya Marais Wastaafu Kupunguziwa Ulinzi

    Gazeti la JAMBOLEO, toleo namba 2381 la tarehe 15 Machi, 2016 limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho "Magufuli awapunguzia ulinzi marais wastaafu".

    Taarifa yake kamili ipo katika ukurasa wa nne, na inaeleza kuwa Mheshimiwa Rais John Magufuli amewapunguzia ulinzi Marais wastaafu na imewataja marais hao kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.

    Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa taarifa hizo sio za kweli na inalitaka gazeti hilo kukanusha habari hiyo mara moja, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

    Aidha, Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa utaratibu wa ulinzi wa Marais wastaafu haujabadilishwa.

    Gerson Msigwa
    Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

    Dar es salaam-15 Machi, 2016
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ikulu Yakanusha Taarifa Ya Marais Wastaafu Kupunguziwa Ulinzi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top