JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua watu watatu
wanaodaiwa kuwa ni majambazi eneo la masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro amesema kuwa
tukio hilo limetokea majira ya saa tatu eneo Masaki Wilaya ya Kinondoni
jijini Dar es Salaam.
Kamishina
Sirro amesema kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa wakati
wakiwa wanajiandaa kufanya tukio la uhalifu katika moja ya ofisi ya
kubadilisha fedha za kigeni iliyopo Masaki.
Amesema
kuwa watu hao walikuwa katika gari lenye namba za usajili T 135 AQJ
aina ya Rav 4 rangi ya Silver, polisi walilisimamisha gari hilo ndipo
majambazi hao wakaanza kurusha risasi na kisha kuzidiwa na kuuawa na
polisi waliokuwa katika doria.
Amesema
baada ya kuwaua majambazi hao walikwenda kukagua na kukuta bunduki
mbili aina ya pisto, Hirizi, Bomu la Kurusha na Mkono pamoja na karatasi
ambayo ilikuwa imeandikwa maneno ya kiaraabu. Sirro amesema
ametangaza kiama kwa watu wanaotumia nguvu katika utafutaji fedha kuwa
hawana nafasi tena katika jiji la Dar es Salaam.
Aidha
amesema kuwa mwandishi, Salma Said aliyetekwa Zanzibar hivi
karibuni ni mzima kutokana na kumkuta kuwa hana jeraha lelote katika
mwili wake.
Amesema
kuwa mwandishi huyo wamechukua malalamiko ambapo wanafanyia upelelezi
juu maelezo aliyetoa baada kuonekana katika mazingira hayo.
Aliongeza
kuwa baada ya upelelezi watachukua hatua lakini kwa sasa yuko katika
matibabu katika Hospitali ya Regency Jiijini la Dar es Salaam.



0 comments:
Post a Comment