https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Mother Teresa kufanywa mtakatifu Septemba


    Mtawa
    Mother Teresa alikuwa mtawa wa kanisa Katoliki
    Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametangaza kwamba Mother Teresa atafanywa mtakatifu Septemba mwaka huu.
    Sherehe ya kumtawaza kuwa mtakatifu itafanyika tarehe 4 Septemba.
    Njia ya kumfanya mtakatifu ilifunguliwa Desemba mwaka jana baada ya Vatican kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kwenye ubongo wake.
    Mother Teresa alipewa tuzo ya amani ya Nobel kutokana na huduma yake kwa raia maskini kwenye vitongoji vya jiji la Calcutta nchini India.
    Alizaliwa 1910 eneo ambalo kwa sasa hujulikana kama Macedonia na wazazi wa asili ya Albania na kupewa jina Agnes Gonxha Bojaxhiu.
    Alipewa uraia kamili wa India baada ya kuanzisha kikundi cha watawa cha Missionaries of Charity mwaka 1950.
    Alifariki 1997 akiwa na umri wa miaka 87. Alifanywa mbarikiwa mwaka 2003.
    Papa
    Mother Teresa na Papa John Paul II wakiwa Kolkata, India tarehe 3 Februari 1986.BBC
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mother Teresa kufanywa mtakatifu Septemba Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top