https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MUUAJI WA WATU 77 MWAKA 2011 NCHINI NORWAY ALALAMIKIA HALI YA GEREZA


    Muuaji wa watu wengi Anders Behring Breivik amepiga saluti iliyokua ikitumiwa na Nazi wakati alipokuwa akiingizwa mahakamani kuwasilisha kesi yake ya kulalamikia hali ya chumba cha gereza alilofungwa huko Norway.

    Breivik, 37, aliyewauwa wau 77 mwaka 2011, hakusema neno lolote alipokuwa akiingia mahakamani, na kuonekana mara ya kwanza kwa umma tangu atiwe hatiani kwa mauaji hayo yaliyoshitua dunia.

    Katika kesi yake hiyo Breivik, amedai amekuwa akitendewa mambo yasiyoyakibinadamu katika gereza la Skien lililopo umbali wa mile 87 kusini magharibi mwa Oslo, ambapo ametengwa kwenye chumba cha peke yake akiwa na komputa na kifaa cha mchezo PlayStation. 
     

    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MUUAJI WA WATU 77 MWAKA 2011 NCHINI NORWAY ALALAMIKIA HALI YA GEREZA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top