Inawezekana
wasanii wakubwa kutoka nchini Nigeria, P.Square ambao sasa hivi wako
nchini South Africa wakishoot video ya ngoma mpya ya Diamond wakaonekana
kwenye ‘reality show’ ya huyo ambayo itaanza kuonekana hivi
karibuni,kwenye
moja ya post zake kwenye page yake ya ‘Instagram’ aliandika kuwa shoo
hiyo sio ‘kireality show’ bali ni ‘reality show’.
‘’Nikisema
sio kireality ina maana kwamba sio tu bora reality,watu wamekuwa
wakisubiria kwa muda mrefu mbali na hivyo pia hata mimi nilikuwa
natamani kufanya muda mrefu lakini nilikuwa nataka vitu vikamilike kama
production kwa sababu ukizungumzia reality unazungumzia production kuwe
na vifaa bora, kuwa na content za kutosha sasa uzuri mie mwenyewe
‘content’ ninazo kwa sababu kila siku nasafiri nina matukio mengi sana
na vitu vingi sana kwahiyo na kupata sponsor ambaye ni mkubwa amabye
anaweza kuingiza hela nyingi inatakiwa iwe imecreatiwa vizuri na kila
kitu, kwa sasa kila kitu kiko sawa,kwahiyo katika step za mwisho ili
kitu kipakuliwe itakuwa online na kwenye tv lakini exclusive zitaanzia
katika moja ya mtandao halafu ndio inaingia kwenye kipindi labda wiki
inayofuata’’Alisema Diamond.
Cloudsfm.com


0 comments:
Post a Comment