Kwa wenzetu nafasi ndio kila kitu, mtu anaweza kuwa na nyumba ndogo lakini alivyoipanga anapata kila kitu tena kwa kuvutia
Nyumba ni mpangilio, nyumba ni mtu mwenyewe…. itategemea wewe unatakaje na unaiwekaje mwisho wa siku ndio unapata kitu unachokihitaji lakini kwanza itapendeza ukiona wengine wamefanyaje ili uibe utundu kutoka kwao, tazama hizi picha hapa chini kama kuna chochote kitakuvutia.
Jiko, dinning na sebule hapohapo na nafasi imebaki…
Hapahapa Tanzania nimeshawahi kuingia dukani na kukuta kitu kama hiki, kama kabati dogo hivi la kuweka viatu kisha unafunga mtu akija haoni kitu
Tulizoea kujiwekea taa za juu lakini hata hii design ya taa za chini kumulika ukuta ni nzuri sana…. na uki-set vizuri hata taa za juu hutozihitaji.
Nyumba inapendeza zaidi nje kama hakuna rangi nyinginyingi na maua mengi, garden simple tu


0 comments:
Post a Comment