Mshambuliaji wa Simba Ibrahimu Ajib amemaliza majaribio yake kwenye klabu ya Afrika Kusini na amefuzu majaribio hayo, kinachosubiriwa kwa sasa ni makubaliano kati kati ya klabu mbili ili biashara ifanyike.
Meneja wa Ajibu Juma Ndambile ameiabia Sports Bar jana usiku kwamba, mteja wake amefanikiwa kufuzu majaribio yake na taratibu nyingine zinafanyika kuhakikisha wanafikiana makubaliano na klabu ya Simba ili imuachie kinda huyo akakipige Bondeni.
“Ajib amefaulu majaribio yake na kwahiyo sasa kilichobaki ni makubaliano kati ya pande mbili, kama mambo yatakwenda sawa basi huenda kijana akacheza Afrika Kusini”.
Jambo la kusikitisha ni kwamba, Ajib aliondoka Simba bila kupewa Baraka na klabu yake huku akimdanganya wakala wake kwamba hana mkataba wowote na klabu yake ya sasa wakati kiuhalisia Ajib bado anamkataba wa mwaka mmoja na Simba.
“Mimi sikua na taarifa za Ajib kuja Afrika Kusini kufanya majaribio, lakini kwasababu mimi nilikuwa nasafari ya kuja huku (Sauz) na yeye akawa anakuja huku basi kama meneja wake, kiongozi na mpenzi wa Simba nikaingilia kati.”
“Endapo kama uongozi wa Simba usiporidhishwa na kitendo alichofanya Ajib kwa kuona alikosea basi ni lazima apewe adhabu anayostahili.”
Meneja wa Ajib hakuitaja moja kwa moja klabu ambayo mteja wake alikwenda kufanya majaribio lakini kwa mujibu wa taarifa zilizopo zinadai nyota huyo alikuwa akifanya majaribio kwenye klabu ya Golden Arrows inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
0 comments:
Post a Comment