https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    AVEVA KATOKA HADHARANI KUANIKA SABABU 4 ZILIZOINYIMA SIMBA VPL

    Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu Simba kuboronga kwenye mashindandao ya msimu huu (VPL na FA Cup) kushoto ni Haji Manara-ofisa habari wa Simba
    Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu Simba kuboronga kwenye mashindandao ya msimu huu (VPL na FA Cup) kushoto ni Haji Manara-ofisa habari wa Simba
    Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva leo May 18 amejitokeza mbele ya  waandishi wa habari na kutoa sababu kadhaa ambazo kwa namna moja au nyingine zimeifanya klabu yao kukosa ubingwa VPL kwa mara nyingine tena ikiwa ni msimu wao wan ne mfululizo bila kutwaa taji hilo.
    Katika hotuba yake kwa wanahabari, Aveva amekiri kwamba malengo yao waliyojiwekea ya kutwaa ubingwa FA Cup na VP yamekwama kwa kushindwa kuchua kombe hata moja kati ya hayo. Badala yake akatumia muda mwingi kueleza sababu ambazo zimefanya Simba kushindwa kufanya vizuri kwenye ligi.
    Wachezaji wameiangusha Simba
    “Kuna wanajeshi ambao hawakuwa tayari kulitumikia jeshi la Simba kwa mfano, kuna mchezaji ambaye kwa makusudi au kwasababu za kimchezo alifanya makosa akafungiwa kutokana na kanuni za mchezo na sisi kama uongozi baada ya kulitathmini hilo tukaona ni lazima tuchukue hatua kali iki kukomesha vitendo kima vile”.
    “Lakini mchezaji huyu hata kabla ya msimu kuisha tayari ameshaondoka na kusaini kwenye klabu nyingine. Hii inaonesha kwa kiasi gani tulikuwa na wanajeshi ambao hawakuwa na uzalendo kwenye jeshi letu”.
    “Wakati tukiwa bado kwenye mapambano, kunamchezaji akafanya rafu ambayo ilikuwa ya kimchezo kabisa lakini inatubidi sasa tuumize vichwa kwamba ilikuwa ni ya kimchezo au makusudi. Baada ya faulo ile, anatoa taarifa usiku wa saa tatu kwamba kesho yake saa nne asubuhi ataondoka kwenda nje ya nchi. Tunajaribu kufanya tathmini kwamba huyu askari alikuwa ni mwenzetu au msaliti”.
    “Wakati bado tukiendelea kuwaza juu ya hayo, kukatokea wachezaji wengine ambao walijaribu kuwashawishi wengine kugomea michezo yote iliyobaki wakianza na mchezo wetu dhidi ya Majimaji”.
    Ushindani mkubwa katika ligi
    “Zamani maisha yalikuwa rahisi sana, unaingia kwenye ligi unamfikiria Yanga pekeyake, wengine unawafikiria kwasababu na wao ni timu. Sasahivi ligi imebadilika, ushindani ni mkubwa, zamani  ilikuwa ni jambo la kawaida kabisa kwenye timu kupokwa pointi kwa kushindwa kufika kwenye kituo cha mchezo kwasababu ya ukata”.
    “Sasahivi timu zile za kawaidakawaida hazipo tena, watu wamewekeza. Kuna Geita, Mwadui, Majimaji na Mbeya City wote hao wanawadhamini”.
    Utendaji mbovu wa TFF
    “Utendaji wao umekuwa sio makini kwa mfano, upangaji mbovu wa ratiba. Kalenda huwa inajulikana mwaka mzima lakini mwaka huu imekuwa tofauti sana, lakini ratiba mbovu imechangia kutuathiri si Simba pekeake lakini pamoja na timu nyingine”.
    Waamuzi
    “Waamuzi wamechangia kwa kiasi kikubwa kuharibu matokeo ya michezo mingi kwenye ligi, si kwa  Simba tu bali hata kwa timu nyingine. Sawa tunakubali wanachukua hatua za kinidhamu lakini lakini zile hatua huwa hazisaidii sana timu kwasababu wakati unamfungia mwamuzi timu inakuwa imeshapoteza ushindi”.

    “Tunapoanza ligi marefa huwa wanawekwa hadharani mapema sana kwamba timu flani itaenda kucheza na timu flani na mwamuzi atakaechezesha mchezo huo. Lakini katika mchezo wetu wa mzunguko wa pili dhidi ya Yanga ambayo alichezesha dadayetu kutoka Bukoba, vilabu havikujua hadi siku mbili au tatu kabla ya mchezo”.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AVEVA KATOKA HADHARANI KUANIKA SABABU 4 ZILIZOINYIMA SIMBA VPL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top