
Harmonize
na Jacqueline Wolper ni couple mpya town. Kwa wengi katika hatua za
mwanzoni walidhani wawili hao si wapenzi bali wanatafuta tu kiki.
Lakini
kadri siku zinavyoendelea kwenda, tumeshuhudia kuwa ni kweli wawili hao
ni wapenzi na wanaonekana kudatishana haswaa. Kuna sababu nyingi
zilizofanya watu wasiamini uwepo wa couple hiyo na kubwa zaidi likiwa ni
miezi michache iliyopita Wolper alichumbiwa na mwanaume mwingine na
tukaamini kuwa sasa mrembo huyo ameamua kuanzisha familia.
Hivyo
baada ya kumuona akiwa na bwana mdogo Harmonize, maswali yalikuwa mengi
ya kuhusu kipi kilichotokea katika uchumba wake na mwanaume huyo.
Na
kwakuwa sasa tunaona kuwa wawili hao wameamua kuuweka wazi uhusiano,
jibu ni kuwa Wolper na mwanaume huyo walivunja uchumba wao. Wolper
anatarajiwa kuzungumza zaidi kuhusu sababu za kuachana mwanaume huyo
tajiri kwenye show ya Take One ya Clouds TV leo usiku.
Sababu
ya pili ni utofauti wa umri kati ya wawili hao. Harmonize ni mdogo mno
kwa Wolper japo wanasema mapenzi hayaulizi kwanini na umri si kitu bali
ni namba tu.

Wakati
ambao kila mtu ameshathibitisha kuwa wawili hao ni wapenzi, baadhi ya
watu wanadhani kuwa mapenzi yao yamekuwa na chumvi nyingi ndani ya muda
mfupi na ni kama wanalazimisha watu waamini kuwa wanapendana.
Katika
wiki mbili hizi, post nyingi za Wolper ni za picha yake akiwa na mpenzi
wake huyo ambaye yeye amuita Raj. “Pale mahaba yanapozidi paka macho
yanaanza kufanana, u have my heart Raj,” ameandika kwenye picha moja.
Harmonize bado ana aibu kiaina kuanika penzi lao lakini amekuwa akitupia
picha mbili tatu za Wolper anayemuita pacha wake.
Lakini
wawili hao wamekuwa gumzo zaidi wiki baada ya kuhudhuria kwenye
birthday ya mtoto wa Aunty Ezekiel na Mose Iyobo, Cookie aliyetimiza
umri wa mwaka mmoja. Wakiwa mbele ya Diamond na wageni wengine waalikwa,
hawakuonekana kutoshana kwakuwa muda mwingi walikuwa wakishikana na
kubadilisha mate bila aibu.
Video
inayowaonesha ‘love birds’ hao wakibadilishana mate hadharani imesambaa
mtandaoni na kuzusha maswali mengi kuhusiana na jinsi wanavyoupeleka
uhusiano wao. Kwa wengi wanaona kama wana show off zaidi na kwamba
uhusiano wao umebeba picha ya kiki kuliko uhalisia wa watu wawili
wanaopendana.
Kwenye
video hiyo Diamond anaonekana kutojali kilichokuwa kikiendelea kulia
kwake wakati kijana wake Harmo alikuwa akishushiana mabusu na mafrench
kiss ya kumwaga na ex wa bosi wake.
“Mkwe leo mmejua kutuchafulia insta… yani kama sabuni ya unga uliyontolea watu MAPOVU,” ameandika Diamond kwenye post yake.

Hata
hivyo kwa showbiz, uhusiano huo utamfaidisha zaidi Harmonize ambaye
anaonekana kufuata nyayo za bosi wake kwa kuziteka headlines kwa story
za uhusiano na mastaa.



0 comments:
Post a Comment