Klabu ya Manchester United bado ipo katika dakika za mwisho kutafuta mbadala wa mshambuliaji wa Mexico aliyekuwa kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Javier Hernandez Chicharito, Man United ambayo August 30 ili muuza Javier Hernandez kwenda katika klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.
Man United walimuuza Javier Hernandez kwenda Bayer Leverkusen kwa dau la pound milioni 12 hivyo wametenga dau la pound milioni 36 ilikuishawishi klabu ya Monaco yaUfaransa kumuachia Anthony Martial ajiunge na wababe hao wa Old Trafford.
Hata hivyo taarifa hizo zinakuja ikiwa ni masaa kadhaa toka Man United ipoteze mchezo kwa goli 2-1 dhidi ya Swansea City, Anthony Martial ambaye analinganishwa kiuchezaji na Thierry Henry alikuwa akiwaniwa na vilabu vya Chelsea na Tottenham Hotspurambayo ilitoa pound milioni 19 kwa Monaco zikakataliwa, bado Man United wanasubiri majibu ya ombi lao la kumnunua nyota huyo.
0 comments:
Post a Comment