https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    HUYU NDO ALIYEIFUNGISHA LIVERPOOL KWENYE FAINALI EUROPA

    Liverpool imepoteza mchezo wake wa fainali dhidi ya Sevilla kwa kufungwa magoli 3 - 1 na Alberto Moreno ndo ameonekana kuiangusha timu.



    Liverpool imepoteza katika mchezo wake wa fainali kombe la Europa jana baada ya kufungwa jumla ya magoli 3 - 1. Kama ilivyokawaida hasa pale timu inapofanya vibaya lazima kuna mchezaji ataonekana kuwa ameiangusha timu kwa kiasi fulani, hilo pia limetokea baada ya mchezo wa jana kumalizika na Liverpool kuruhusu kipigo cha magoli 3 kwa moja ambapo lawama zote zimeelekezwa kwa Beki wa kushoto Alberto Moreno.

    Mchezaji wa Zamani wa Liverpool Jamie Carragher alishaonyesha wasiwasi wake na mlinzi huyo na wasiwasi wake umebainika wazi katika mchezo wa jana.
    Maneno aliyoyaandika Jamie Carragher yakiashiria kutokufurahishwa na kiwango cha Beki wa Kushoto wa Liverpool


    Moreno alionekana kutokujua majukumu yake uwanjani hapo kwa kutoka mara kwa mara katika nafasi yake kitu kilichopelekea washambuliaji wa Sevilla kupenya kirahisi kupitia upandde wake. katia hatua hiyo muhimu katika mchezo wa soka Alberto Moreno amefanya zaidi ya makosa 40 yaliyoigharimu timu yake. 

    Liverpool walienda mapumziko wakiwa vifua mbele lakini mambo yalibadilika ghafla tu kilipoanza kipindi cha pili. Dakika 15 na sekunde 17 baada kipyenga cha half time Liverpool walijikuta wakisawazishiwa goli walilokuwa wanaongoza huku Moreno akishika mikono yake kiunoni na kuzitazama tatoo zake zilizojaa mikononi, alipiga kichwa lengo likiwa ni kuokoa mpira ila mpira huo ulimfikia beki wa kushoto wa klabu ya Sevilla akamchenga moreno na kupiga krosi iliyomaliziwa vizuri na Gameiro na kufanya mchezo kuwa 1 - 1. 
    Moreno akiwa amehuzunishwa baada ya Sevilla kusawazisha

    Moreno pia alikuwa akipanda sana mbele kwenda kushambulia na kusahau majukumu yake kama beki. Goli la pili la Coke lilifungwa wakati Moreno akiwa hayupo kabisa katika nafasi yake ambayo angeweza kuzuia mashambulizi ya wapinzani.
    Moreno akipeana mkono na kocha wake baada ya mechi kuisha
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HUYU NDO ALIYEIFUNGISHA LIVERPOOL KWENYE FAINALI EUROPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top