Mchezaji wa Dinamo Bucharest, Patrick Ekeng, amefariki dunia baada ya kupatwa na shambulio la moyo na kuanguka uwanjani.
Ekeng ambaye pia ni kiungo wa timu ya taifa ya Cameroon alianguka uwanjani dakika ya 70 ya mchezo wa ligi ya Romania baina ya Dinamo na Viitorul.
Saa mbili baadaye ilielezwa kuwa Ekeng amefariki dunia hospitalini baada ya kukimbizwa kwa matibabu zaidi.




0 comments:
Post a Comment