
Hivi karibuni familia ya WCB
imeonekana kuchafua hali ya hewa mitandaoni baada ya picha zilizokuwa
zinasambaa zikionyesha couple hiyo mpya mjini kati ya Jacqueline Wolper
na Harmonize huku baadhi ya mashabiki wakisema kuwa ilikuwa ni kiki
lakini kwa sasa mambo yanaonekana kubadilika.
Akiongea kwenye kipindi cha Take
One, kinachoruka kupitia Clouds TV, Wolper alisema kuwa anaweza akawa na
mwanaume anayefanya kazi yeyote sababu haitaji pesa kutoka kwa
mwanaume.
“Naweza hata nikawa na mtu
anaendesha bodaboda au anaweza sijua akawa mfagia hoteli, sijui anafagia
nini lakini mimi kama mimi nikambadilisha na akawa mwanaume wangu. Kwa
sababu nachokihitaji mimi sihitaji pesa mimi ni mpiga kazi, mimi nafanya
kazi na ndiyo maana mwanzo nimeanza like na fanya promosheni Napata
hela yangu, sitaki kutegemea mtu,” aliongeza.
Wolper alianzisha uhusiano na
muimbaji huyo wa ‘Bado’ baada ya kuvunja uchumba na mwanaume aliyeahidi
kumsomesha nchini Afrika Kusini na ambaye alikuja kugundua kuwa ni mume
wa mtu.


0 comments:
Post a Comment