ZIKIWA
zimesalia siku chache kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kuanza, staa
wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ jana aliukaribisha kwa kula chakula
cha jioni na watoto yatima.
Nisha
aliwatembelea watoto yatima wa kituo cha New Hope Family Group
kilichopo Kigamboni, Dar, ambapo alipata nafasi ya kula nao chakula cha
jioni alichokiandalia, hali iliyosababisha watoto hao kufurahia
vilivyo.
Akizungumza
kituoni hapo, Nisha alisema ameamua kushiriki na watoto hao chakula
hicho ili kuukaribisha mwezi mtukufu kwani atasafiri nje ya nchi hivyo
akaona ni vyema kuwaachia japo msaada wa chakula na mahitaji mengine.
“Nawapenda
sana watoto yatima na kila mwisho wa mwezi huwa nakuja kuwaona, mwisho
wa mwezi huu mpaka Ramadhan inaanza sitakuwepo ndiyo maana nimekuja
leo,” alisema Nisha.


0 comments:
Post a Comment