Lema ambaye ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya nchi ameyasema hayo
katika mahojiano maalum na EATV kuhusu maamuzi ya Rais kumng'oa Waziri
Kitwanga katika wadhifa wake ambapo Lema amebainisha wazi kwamba Rais
alipaswa kutengua uteuzi wa waziri huyo baada ya kuandamwa na kashfa ya
ufisadi kwa kampuni ambayo ana ubia nayo ambayo ilipewa kazi ya kufanya
manunuzi na kuweka mashine za kuhifadhi alama za vidole katika vituo vya
polisi nchini.
''Bunge lilipuuzia maoni ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu suala la Waziri Kitwanga kuhusika katika kampuni iliyopewa kazi ya kuweka mashine katika vituo vya polisi, kama Rais alikuwa na nia njema angemsimamisha mapema kupisha uchunguzi, hii ya kuja kumsimamisha kwa maadili ya unywaji pombe ni issue ndogo ukilingnisha kashfa ya lugumi''-Amesema Lema.
Aidha Mbunge huyo ameeleza kuwa wakati wa Bunge la katiba pombe ilikuwa inauzwa bungeni hivyo kitwanga kusimamishwa kachukuliwa kama sample tuu kwakuwa wabunge na mawaziri wanaokunywa pombe wakati wa kazi ni wengi zaidi.

0 comments:
Post a Comment