Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa
na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais
Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R.
Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi.
Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt.
Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa
Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu
wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu
kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa
watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya
139.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais
Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa
wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe.
Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo
itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika
uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi
zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa
halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha,
nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine
ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye
elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa).



0 comments:
Post a Comment