Jana aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa lengo la kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na kutaka arejeshwe katika nafasi ya uenyekiti aliyokuwapo awali.
Prof. Lipumba alijiuzulu kuwa mwenyekiti wa CUF tarehe 6 Agosti 2015 siku chache baada ya CHADEMA kumkubali aliyekuwa mgombea wa urais Edward Lowassa kujiunga na umoja huo (UKAWA) na kuchukua fomu ya kugombea urais. Prof. Lipumba alijiuzulu kwa kusema kuwa nafsi yake inamsuta kwani wamemkaribisha mtu waliyempiga vita miaka mingi.
Jana tarehe 13 Juni 2016, Prof. Lipumba aliandika barua akitaka kurejeshwa katika wadhifa huo baada ya kusikia kuwa CUF kimetangaza uchaguzi ili kuweza kuziba nafasi zilizoachwa wazi.
Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif amesema kuwa, Prof. Lipumba atafute uenyekiti wa chama kingine chochote kwa sababu hana nafasi CUF.
Maalim Seif alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari nchini Marekani aliyetaka kujua maoni yake kuhusu barua hiyo ya Prof Lipumba.


0 comments:
Post a Comment