Headline
kutoka bungeni Dodoma June 02 2016 kazi ilikuwa ni maswali na majibu
kutoka kwa wabunge kuielekezea Serikali, kazi ya ufafanuzi ilikuwa
ikitolewa na Mawaziri. Wabunge mbalimbali waliipata nafasi hiyo ya
kuwasilisha maswali yao, lakini hii ya Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe yeye alisimama kutoa taafifa rasmi.
Hapa anasema…>>’Leo
saa tisa usiku katika soko kuu la wilaya ya Nzega kumetokea moto mkubwa
ulioteketeza baadhi ya maduka ya wafanya biashara, lakini hoja yangu ni
kwamba kwa miaka mitano wamekuwa wakilipa ushuru wa zima moto na
taasisi hii imeshindwa kuwapatia huduma wananchi.
‘Sasa
nataka tujadili kwa pamoja pale ambapo mwananchi anatimiza wajibu wake
wa kidheria wa kulipia huduma kwenye taasisi na taasisi hiyo inashindwa
kumpatia mwananchi huduma. Je, ni halali wananchi kuendelea kulipa
ushuru wakati hawapewi huduma stahiki‘


0 comments:
Post a Comment