https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    POLISI WASEMA MTU MMOJA TU ALIHUSIKA KATIKA SHAMBULIZI LA MUNICH

    Shambulizi la kutumia bunduki Jijini Munich katika duka la bidhaa lililouwa watu tisa limefanywa na mtu mmoja mwenye silaha ambaye naye alijiuwa, polisi wa nchini Ujerumani wamesema.

    Polisi wameviambia vyombo vya habari kuwa mtuhumiwa aliyetekeleza shambulizi hilo ni kijana wa miaka 18 mwenye Uraia wa Ujerumani na Iran ambaye alikuwa akiishi Munich, hata hivyo haijajulikana dhamira ya shambulizi hilo.

    Katika shambulizi hilo watu 16 walijeruhiwa na watatu miongoni mwao wakiwa mahututi, huku msako ukianzishwa kufuatia ripoti kuwa zaidi ya watu watatu wenye silaha walihusika na shambulizi hilo.
        Mwili wa mtu aliyeuwawa kwa kupingwa risasi ukiwa umefunikwa kwa shuka jeupe
    Kituo cha matibabu ya dharura kikiwa kimejengwa kwa muda ili kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: POLISI WASEMA MTU MMOJA TU ALIHUSIKA KATIKA SHAMBULIZI LA MUNICH Rating: 5 Reviewed By: news
    Scroll to Top