Polisi walioshehena silaha nzito maalum kwa ajili ya kufanya doria wamesambazwa rasmi kwenye mitaa ya Jiji la London nchini Uingereza hii leo baada ya wimbi la matukio ya mashambulizi ya ugaidi Ulaya.
Kamishina wa polisi Sir Bernard Hogan-Howe amebainisha mpango ambao licha ya kuweka askari wenye sare pia kutakuwa na askari kanzu wanaofanya doria wakiwa na bastola na bunduki ya SIG Carbine rifles.
Mbali na bunduki polisi hao wapya wa doria watakuwa na pikipiki aina ya BMW F800GS ili kuwaruhusu kulifikia kwa urahisi eneo lolote na katika Jiji Kuu kutakuwa na bodi za mwendo kasi zitakazokuwa zikifanya doria.
Polisi maalum wa kupambana na ugaidi wakiwa na vifaa vyao kama vinavyoonekana katika maelezo kulingana na namba





0 comments:
Post a Comment