Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa ufunguzi wa
mashindano ya Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 30, 2016.(PICHA NA LORIETHA LAURENCE WHUSM)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akifyatua baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Vyama vya
Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) leo JijiniDar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa ufunguzi wa
mashindano ya Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 30, 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akitoa salamu kwa wanamichezo ambao ni walimu wanaowakilisha nchi za
kusini mwa Afrika wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo jijini Dar es
Salaam. Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi
za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kushoto ni Rais wa Chama cha
WaalimuTanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.
Rais wa Chama cha Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika
(SATO) Bw. Henry Kapenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja
wa Vyama vya walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar
es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye, na kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw.
Gratian Mukoba.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian
Mukoba akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa
Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye (katikati) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa mashindano
ya michezo inayoshirikisha Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika
(SATO), wa pili kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw.
Gratian Mukoba, na kushoto ni Katibu kutoka Ofisi ya Uhamiaji wa Ubalozi wa
Malawi Bw. Michael Gama. Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya
Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kulia ni Katibu
Mkuu wa chama hicho Bw. Richard Gundane.
Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Afrika ya Kusini wakiingia
uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.
Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Zambia wakiingia uwanjani
wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC) leo JijiniDar es Salaam.
Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Tanzania wakiingia uwanjani
wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC) leo Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Brass Bendi ya Polisi Nchini wakiongoza maandamano ya
wanamichezo ambao ni walimu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kuingia uwanjani
wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment