Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu wa pili kushoto akitoa maagizokwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai wa kwanza kulia
wakati alipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu katikati akimfariji mtoto Rahel Razaro wa kwanza kushoto
aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) alipotembelea
wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam na wa kwanza
kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo Dkt. Samuel Swai.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali
chini ya Wizara ya Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
imeitaka Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) kuhudumia wagonjwa haraka
iwezekanavyo ili kuondoa msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo na
kuwaruhusu wakaendelee na shughuli za kujenga taifa.
Akizungumza
hayo alipotembelea wagonjwa MOI Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,
Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliwataka watumishi wa
taasisi hiyo kuwahudumia wagonjwa haraka iwezekanavyo ili kuwapa fursa
ya kwenda kufanya shughuli za kimaendeleo kwa ajili ya taifa.
“Mnatakiwa
kuhudumia wagonjwa kwa haraka na ufanisi mkubwa ili kuwasaidia
watanzania kutotumia muda mwingi wakiwa hospitalina na badala yake
wapone waende wakaendelee na shughuli zao za kujenga taifa kwa maendeleo
ya Nchi yetu”alisema Mhe. Ummy
Aidha
Mhe. Ummy ameongeza kuwa licha ya kuwa na changamoto zinazojitokeza
hospitalini hapo Wizara ipo bega kwa began a Taasisi hiyo kuhakikisha
huduma bora zinatolewa kwa wananchi chini ya kitengo hiko ili kufikia
malengo ya milenia.
“Nafahamu
kama kuna changamoto zinazoikabili taasisi hii kama mlivyonieleza
lakini tupo pamoja katika kuziondoa na nyinyi hakikisheni mnafanya kazi
kwa bidii ili kuondoa malalamiko ya wananchi na kuleta huduma bora na
kwa wakati” alisisitiza Mhe. Ummy.
Mbali
na hayo Mhe. Ummy ameitaka taasisi hiyo kurudisha huduma ya kufanya
upasuaji kwa wagonjwa siku za jumamosi bila ya kukosa tena kwa haraka
ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa kwenye taasisi hiyo.
Kwa
upande wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji MOI Dkt. Samuel Swai amesema kuwa
wamepokea agizo hilo na wapo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa
maisha ya watanzania kwa haraka na ubora zaidi.
“Tupo
tayari kutekeleza agizo la Mheshimiwa Waziri la kufanya kazi kwa bidii
ili kuokoa maisha ya watanzania kwa haraka na ataona matokeo mazuri
kuanzia leo hii” alisisitiza Dkt. Swai.


0 comments:
Post a Comment